Video: Charlene Ruto akionesha umahiri katika kutafsiri kwa lugha ya ishara

Video hiyo inamuonesha Charlene Ruto akiwa kwenye jukwaa kando ya msemaji ambaye alikuwa akisema maneno kwa kutumia kipaza sauti na Charlene akiyatafsiri kwa lugha ya ishara.

Muhtasari

• Sasa binti huyo wa kwanza wa taifa ameonesha weledi na umahiri wake katika kutumia mafunzo hayo ya miezi mitatu kutafsiri mahubiri kwa lugha ya ishara mbele ya umati wa watu.

Charlene Ruto.
Charlene Ruto.
Image: X

Wiki moja iliyopita, Radio Jambo tulibaini kwamba binti wa kwanza wa taifa Charlene Ruto alifuzu kutoka chuo baada ya kozi ya miezi mitatu ya mafunzo ya lugha ya ishara.

Sasa binti huyo wa kwanza wa taifa ameonesha weledi na umahiri wake katika kutumia mafunzo hayo ya miezi mitatu kutafsiri mahubiri kwa lugha ya ishara mbele ya umati wa watu.

Katika video ambayo ilipakiwa kwenye chaneli ya mkuza maudhui Vincent Mboya, Charlene Ruto alionekana amesimama mbele kwenye jukwaa kando ya msemaji ambaye alikuwa na kipaza sauti mkononi akimzungumzia na wakati huo huo Charlene akijaribu kutafsiri kile kilichosemwa kwa njia ya ishara.

Japo hakukuwa na maelezo Zaidi kuhusu mkutano huo, inaaminika kwamba walikuwa wakizungumzia kuhusu jinsi ya kuwa na mawasiiano faafu na watu ambao hawana uwezo wa kusikia na njia pekee ya kufanikisha mawasiliano nao ni kupitia lugha ya ishara.

“Niliona machapisho mengi, kwa hiyo niliketi na kuyasoma yote. Mmoja aliniandikia na kuniuliza kuhusu jamii ya viziwi, hiyo barua iliuwa na siku ya mkutano, na ningependa kuelewa Zaidi kuhusu jamii ya watu viziwi,” sehemu ya maneno ya msemaji ambayo Charlene alijaribu kutafsiri kwa lugha ya ishara yalisemwa.

Wakati wa kufuzu kwake Charlene Ruto alidokeza kwamba alikuwa ameshiriki masomo hayo kwa kipindi cha miezi mitatu.

“Baada ya miezi 3 ya kusoma Lugha ya Ishara ya Kenya (maarufu kama KSL) kama kozi ya msingi, hatimaye nilihitimu na cheti changu!” alisema.

“Sikuweza kujivunia zaidi yangu! Nilipokutana na Babelyn Mukila mapema mwaka huu na aliwasiliana nami kupitia KSL pekee na ilizua shauku yangu si tu katika lugha bali zaidi kwa vijana Viziwi, jumuiya ya Viziwi na utamaduni wa Viziwi. Nimekuja kukuza shauku na upendo kama huu kwa Viziwi,” aliongeza binti Ruto.

Tazama video hii akitafsiri kwa lugha ya ishara