Mwelekezi na mtayarishaji wa filamu na tamthilia Lamata Lea nchini nchini Tanzania, Lamata Leah ameweka wazi jinsia ya mtoto anayetarajia kujifungua.
Hili ameliweka wazi katika video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagramu ambayo aliwashirikisha mastaa wengi zaidi kwenye sherehe hiyo ya kuweka wazi jinsia ya mtoto ambaye anatarajia kujifungua.
Kupitia ujumbe huo unaonyesha kuwa mtoto ni wa kiume, jambo ambalo limepokelewa kwa furaha kubwa si kwake tu bali hata kwa rafiki zake wakiwemo wasanii na waigizaji ambao ni mastaa kwenye tasnia ya sanaa.
Video aliyoichapisha kwenye huo kurasa iliambatana na ujumbe uliojawa na furaha na shukrani tele uliosoma;
"Latema sehemu ya 2 ni Msichana au Mvulana?✨️Mungu ametenda🙏✨️Kwanza kabisa napenda kumshukuru mungu kwa ukuu wake 🙏❤️ pili nipende kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki kwa kuweza kufanikisha Gender reveal hii mwenyezi mungu awabariki sana 🙏."
Aliendelea kuonyesha furaha yake na jinsi anavyomsubiri mwanaye kwa hamu zaidikama mzazi na kuwataja wote aliofanikisha siku hiyo.
"Siwezi kusubiri kukuona mtoto wangu wa kiume 😍💙💙,Shukrani z kipekee🙏 kwa; @lutwilu_events,@ossy_coctails,@ivafluffycakes,"mimi_mvrs11,@cherehani1,@romyjoans,@official_djangie,@doraofficial na @lamata village studios.
Kwenye hafla hiyo ya taarifa njema marafiki na msataa waliofika walitunuku zawadi mbali mbali kama njiamojawapo ya kuonyesha furaha yao na kumpongea swahiba huyo ambaye ni mtajariwa.
Latema anatambulika zaidi katika tasnia ya sanaa na kuongoza vipindi vya bongo hasa kile cha JUAKALI ambaco kinafanya vizuri sana kwenye uigizaji.
Ni mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Latema Village entertainment, ambayo imeibua na kufanya kazi na vipaji vingi ndani na nje ya Tanzania.