Nikianza kutumbuiza nilikuwa natumia chupa za maji kama maikrofoni - Mbosso

“Mkubwa alikuwa anatupa chupa za maji hizi unazoziona, alikuwa anatupa unatumbuiza Mkubwa anakuangalia unavyotupa mikono kushoto na kulia, kuwa mtumbuizaji," Mbosso alisema.

Muhtasari

• Msanii huyo alikumbuka kwamba wakati Mkubwa Fella anawafunza jinsi ya kutumbuiza, alikuwa anawapa chupa za maji.

Mbosso.
Mbosso.
Image: Insta

Mbosso Khan kwa mara ya kwanza amefunguka jinsi alivyoanza safari yake ya muzki mikononi mwa mdau mkubwa sana wa muziki nchini Tanzania ambaye anamuita kama babake katika Sanaa, Mkubwa Fella.

Akizunugumza baada ya mafanikio makubwa ya shoo yake ya mkoa wa Songea alipoingia jukwaani aliwa amejifunga taulo, Mbosso alisema kwamba mafanikio yake yote hayatokani na Wasafi bali ni kwa Mkubwa Fella ambaye ndiye mtu wa kwanza kukitambua kipaji chake na kumpa nafasi ya kukionesha kwa ulimwengu.

“Mkubwa Fella ni baba wa kazi mimi amenilea na amenikuza. Ni mwalimu aliyenifunza muziki. Kwa hiyo mpaka leo hii unauona Mbosso, ni Mkubwa Fella kwanza ndio kafika kwa Mbosso. Akiniona ninatumbuiza, nafanya vizuri, yeye hanioni kuanzia pale mnakoniona nyinyi, ananiona kuanzia steji yangu ya kwanza ya kukua,” Mbosso alisema.

Msanii huyo alikumbuka kwamba wakati Mkubwa Fella anawafunza jinsi ya kutumbuiza, alikuwa anawapa chupa za maji kuzitumia kama vipaza sauti na baadae akawapaisha kutumbuiza kwa umati mdogo mdogo bila maikrofoni.

“Mkubwa alikuwa anatupa chupa za maji hizi unazoziona, alikuwa anatupa unatumbuiza Mkubwa anakuangalia unavyotupa mikono kushoto na kulia, kuwa mtumbuizaji, tukaendelea tukawa paka tukapata vifaa vya bendi tukaanza kutumbuiza bila maikrofoni. Tulianza nikiwa miaka 16 mpaka sasa hivi nakaribia miaka 28 sio mchezo,” Mbosso alifichua.