Nikionekana nawe wanasema unataka kunipa sumu - Ommy Dimpoz amwambia Diamond

Dimpoz aliashiria kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawapendi kuona wakiwa wanatabasamu na Diamond kwani watafanya wawezalo kuibua figisu.

Muhtasari

• Alimtaja Mange Kimambi ambaye anaishi Marekani na muda wote amekuwa mkosoaji mkubwa wa mitikasi ya Diamond.

Ommy Dimpoz,
Ommy Dimpoz,
Image: Instagram

Marafiki wa tangu jadi Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz kwa mara nyingine wamezua gumzo mitandaoni baada ya Diamond kupakia klipu wakiwa wananong’onezeana katika hafla moja.

Diamond kupitia Instagram yake alipakia klipu hiyo akiwa ananong’onezewa na Ommy Dimpoz karibu na sikio lake huku Diamond akiachia tabasamu hadi magego kujianika nje.

“Mandugu tangia siu ya kwanza,” Diamond aliandika.

Ila alichokojibu pale Ommy Dimpoz kilivutia hisia nyingi kutoka kwa mashabiki wa wasanii hao walipleta mabadiliko na mageuzi makubwa katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Ommy Dimpoz ambaye alinusurika kifo baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na kile baadhi walidai ni kulishwa sumu alisema kwamba kuna baadhi ya watu wabaya ambao hawapendi kuona wasanii wakiwa pamoja.

Msanii huyo wa Tubogo alisema kuwa baadhi ya wabaya hao wakiona klipu hiyo wataanza kusema Diamond anapanga njama ya kumwekea sumu tena.

Alimtaja Mange Kimambi ambaye anaishi Marekani na muda wote amekuwa mkosoaji mkubwa wa mitikasi ya Diamond.

“Basi Mange Kimambi akiamka na kuona hii atasema unataka kunipa sumu,” Ommy mwenye utani alisema.

Itakumbukwa kwa kipindi Fulani wasanii hao ambao walikuwa marafiki walifika wakakosana na kutupiana majipu makali usoni kiasi kwamba hawakuwa wanaonana ana kwa ana.

Lakini ndio hivyo tena, baada ya Ommy kupona, alikuja akarekebisha uhusiano wake na Diamond na japo hawajaonekana pampoja kwa ukaribu ule wa awali, wameweza kurekebisha ubaya ulichomoza na sasa wanaitana kaka.