- Aidha alifichua kuwa kuna familia nyingi nchini Kenya zinazokabiliwa na masuala kama hayo hata hivyo hali yao si dhahiri kwa vile wao si watu mashuhuri kama wao.
Seneta mteule Karen Nyamu kwa mara nyingine ametoa maoni yake kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu yeye na Edday Nderitu.
Karen Nyamu ambaye alikuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha redio nchini alifichua kuwa mazungumzo hayo yalimfanya aonekane kama mwanamke mbaya sana.
”Unajua kuna conversation inanendelea nikae kama mimi sio mtu mzuri nina roho mbaya na sio hivyo”
Seneta huyo wa ambaye alinaswa katikati ya msukumo mbaya na vuta nikuvute na Edday Nderitu kwa ajili ya msanii maarufu wa mugithi samidoh alifichua ugumu anaokumbana nao wakati akijaribu kuzuia suala hilo.
"Nimejaribu kupanga mambo ya roho nikashindwa," Karen Nyamu alisema na kuongeza kuwa katiba ya Kenya inatambua ndoa za wake wengi.
”Na isitoshe sheria yetu inaruhusu polygamus marriage, si lazima mmoja aondoke ndo mwengine abaki” Nyamu alisema wakati wa mahojiano.
Aidha alifichua kuwa kuna familia nyingi nchini Kenya zinazokabiliwa na masuala kama hayo hata hivyo hali yao si dhahiri kwa vile wao si watu mashuhuri kama wao.
Mbunge huyo ambaye ni shabiki namba moja kabisa wa Samidoh hata hivyo alishangaa ni kwa nini wengi huchukizwa anapojitokeza kwenye tamasha za mpenzi wake.
Mume wangu ni Msanii mkubwa katika nchi hii, na ni furaha yake namba moja.. kwa hivyo nikimfuata bwanangu kwenye tour zake, namkosea nani”
Mama huyo wa watoto watatu anasema ana nia njema zaidi na kutofautina na jina amabalon alikuwa amepewa na mashabiki mitabndaoni 'Home wrecker'
"Mimi nina imani sana.. hata kama itachukua mwaka, itawork. Kwa sababu roho na nia iko mahali pazuri," Karen alisema.
Huku akikiri kwamba huenda hakushughulikia hali hiyo vyema, Karen Nyamu alisema matumaini yake ni familia zote mbili kuwa na furaha.