'Usiufunue utupu wa mamako, ni dhambi!' Mchungaji alaani vijana kuoa bibi wazee

‘Usiufunue utupu wa mama yako’ Biblia imeandika kwenye mambo ya Walawi. Mama yako si lazima yule tu aliye kuzaa, ni yule aliyekuzidi umri" mchungaji huyo alisema.

Muhtasari

• Alitumia nadharia ya mchuzi na nyama na kuwataka vijana hao wanaokwenda na mtindo wa kufuata pesa kwa kina mama wazee.

Rev Richard Hananja.
Rev Richard Hananja.
Image: Insta

Mchungaji mmoja kwa jina Hananja ameingilia kati suala la vijana wadogo ambao wamekuwa na mienendo ya kutoka kimapenzi na kina mama wanawazidi umri mara dufu.

Katika klipu hiyo, mchungaji huyo anasema kwamba kijana wa miaka 20 kuoa bibi wa miaka 70 kwenda mbele ni dhambi wala si fasheni ya maisha ya kisasa kama ambavyo imechukuliwa mijini.

Mchungaji Hananja alikwenda mbele na kunukuu kifungu katika Biblia ambapo alihubiri akisema kwamba si maneno yake bali ni maneno ya Mungu kwamba kuufungua utupu wa mwanamke aliyekuzidi umri ni sawa sawa na kuufungua utupu wa mama yako – ni dhambi!

“Kijana wa miaka 20 anaoa bibi wa miaka 70, hiyo hapana, kwanza hiyo ni laana. Kibiblia hiyo ni dhambi. ‘Usiufunue utupu wa mama yako’ Biblia imeandika kwenye mambo ya Walawi. Mama yako si lazima yule tu aliye kuzaa, ni yule aliyekuzidi umri. Au baba yako aliyekuzidi umri, ni dhambi Kibiblia, ni laana,” mchungai Hananja alisema.

Alitumia nadharia ya mchuzi na nyama na kuwataka vijana hao wanaokwenda na mtindo wa kufuata pesa kwa kina mama wazee kwa ajili ya mapenzi kuchagua nyama [wasichana] kuliko kuchagua mchuzi [mama wazee].

“Wasichana si wako wengi tu, unakwenda kuchagua mchuzi wakati nyama zipo. Kusema unakwenda kwa ajili ya maslahi, hivyo ni vitu vinaweza vikapita tu, na kijana usitake kutunzwa, jitafutie. Ukisema unataka kutunzwa huo ndio unyonge na uvivu duniani. Na ukiwa hivyo unaweza ukafanyiwa chochote ujue. Tafuta za kwako, maisha ya kutafuta pamoja ndio maisha matamu,” mchungaji alisema.