Ni njaa mingi huyu-KRG amwambia Cassypool

"Namuelewa najua ni njaa ,usijali tutakuleta mjini na tutakusaidia ukiamua kukaa karibu nasisi."

Muhtasari

•KRG,alimkosoa Cassypool kwa kueneza porojo mitandaoni kumhusu na hivyo kumwambia apunguze mwendo wa kueneza porojo ili walete maelewano kati yao

KRG the Don,Cassypool./Instagram
KRG the Don,Cassypool./Instagram

Msanii Karuga Kimani almaarufu KRG the Don, amekutana na mwandani wake Cassypool baada muda wa kurushiana cheche za maneno.

Wawili hawa walipatana  kwenye kongamano la wanablogu katika hafla iliyoandaliwa ya kuwahamasisha kuhusu Watanashati Festival ambayo itafanyika Kaunti ya Meru mnamo Octoba 7 mwaka huu.

KRG,alimkosoa Cassypool kwa kueneza porojo mitandaoni kumhusu na hivyo kumwambia apunguze mwendo wa kueneza porojo ili walete maelewano kati yao.

"Cassypool amejisasa sana najua ameongea mambo mengi,mengi ya matusi lakini hayo ni mambo madogo ya siasa na porojo zako ila namuelewa najua ni njaa ,usijali tutakuleta mjini na tutakusaidia ukiamua kukaa karibu nasisi."

Amesema lengo kuu la kuandaa onyesho hilo ni kuwaburudisha, kuwaelimisha na kukuza talanta za vijana wa Meru ili nao wapate nafasi ya kueneza vipaji vyao akisema kwamba vijana wenye talanta watapewa kipaumbele.

Kama njia moja ya kuwatia moyo vijana na mashabiki kushuriki katika hafla hiyo amesema watakaojitokeza kwenye onyesho hilo watapewa pesa kidogo za kuwakaribisha.

Cassypool ambaye alionekana kukana matamshi ya KRG ya kumtemea cheche za maneno alisema ni watu tu wanataka kuwakosanishana kuharibu uhusiano wao wa karibu.

Hivi karibuni kumeshuhudiwa kurushiana kwa maneno ya uhasama miongoni mwa wasanii wa muziki wa injili, hasa ya kulaumiana kwakile wanachodai kuwa tasnia hiyo ya muziki inaonekana kufifia.

Hivi majuzi, wakati Eric Omondi akimlaki msanii wa injili kutoke Tanzania Christina Shusho, alionekana kusema kwamba tasnia ya muziki wa injili imefifia na kusem kuwa wasanii ambao wanafanya vizuri kwenye muziki huo ni wachache zaidi akimtaja mercy Masika kama msanii ambaye anafanya vyema.