logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wacha kila mtu aishi Maisha yake - Amberay asema kuhusu Vera na Mauzo kuachana

Siku chache baada ya wawili hao kuachana

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 September 2023 - 14:29

Muhtasari


  • • Amesema kwamba,ili kufikia mtu kuchukua hatua ya kuamua kuachana katika ndoa, basi anjua kile ambacho labda anakipitia kwenye ndoa.
Amberay/Instagram

Amberay anayejulikana kama Faith Makau jina lake halisi,ametoa maoni yake kuhusu kutengana kwa msanii Vera Sidika na aliyekuwa mpenzi wake Brown Mauzo.

Amesema kwamba,ili kufikia mtu kuchukua hatua ya kuamua kuachana katika ndoa , basi anajua kile ambacho labda anakipitia kwenye ndoa.

"Mwacheni jamani, huwezi kujua amekua akipitia nini,wacha kila mtu aishi maisha yake."

Hata hivyo amesema kwamba awezi akafurahikia jambo la wawili hao kutengana,ila anawatakia kila la heri kwenye maisha yao ya baadae.

"Siwezi kusherehekea watu kuachana,ila wao ndio wanajua tatizo lilikua wapi. Langu ni kuwaombea na kuwatatkia mema kwa masiha yao."

Alieleza kuwa wawili hao ni watu wazima na wazazi, hivyo kwa hakika mwishowe lazima watapata suluhu kwa tatizo la ndoa lililopelekea wao kutengana

Akiwa kwenye mazungumzo ya moja kwa moja na SPM BUZZ,alikwepa kujibu swali kuhusu drama za Rapudo akisema kwamba hapendi kuzungumzia maswala ambayo kwa wakati mwingine ajihisi kuyazungumzia.

Amesema kwamba ni mengi yamekuwa yakitendeka lakini, anamushukuru mMungu kwa kumwezesha kusimama imara na kuwa alivyo.

Katika mazungumzo hayo, amemtakia mwimbaji Melina Gold mema akisema kwamba ako na matumaini tele kwamba taipeleka yasnia hiyo ya muziki kwa hatua kubwa sana akisema alifanya vyema katika wimbo wake.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved