logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee amualika Beyonce katika sherehe yake kufuzu chuo kikuu baada ya miaka 14

"Nitag msanii unayempenda niwe naye kwenye mstari wa burudani" alisema.

image
na Radio Jambo

Makala24 September 2023 - 06:40

Muhtasari


• “Hatimaye nitahitimu Desemba baada ya miaka 14 ya mapambano ya kukamilisha shahada yangu ya usimamizi wa Biashara." Akothee.

Akothee kumualika Beyonce mahafali yake.

Akothee amefichua kwamba baada ya kung’ang’ana kutafuta digrii yake ya kwanza kwa kipindi cha miaka 14 chuoni, hatimaye anatarajia kufuzu mwezi Desemba mwaka huu.

Msanii huyo alifichua haya dakika chache baada ya kuhushuria sherehe ya mahafali ya mwanawe wa kiume Evander Holifield ambaye alifuzu kwa digrii ya uhandisi baada ya miaka 5 chuoni.

Kinyume na mwanawe ambaye amechukua miaka 5 tu kupata digrii, Akothee safari yake haijawa rahisi kwani alilazimika kufukuzia digrii hiyo kwa miaka 14 na hatimaye anapotarajiwa kufuzu, amedokeza kwamba huenda akaandaa sherehe kubwa tena ya kukata na shoka itakayohudhuriwa na mastaa wenye haiba ya nyota tano.

Msanii huyo wakati anawauliza mashabiki na wafuasi wake ni wasanii wapi wangependa awaalike, mwenyewe alidokeza kwamba huenda atamualika msanii wa kimataifa Beyonce kama mgeni wa heshima.

“Hatimaye nitahitimu Desemba baada ya miaka 14 ya mapambano ya kukamilisha shahada yangu ya usimamizi wa Biashara. Je, umealikwa? Nitag msanii unayempenda niwe naye kwenye mstari wa burudani. Ninafikiria kumualika Beyonce. Hii ni kubwa,” alisema.

Akothee alifichua kwamba atafuzu kutoka chuo kikuu cha Mt Kenya na akasema kwamba alichagua kozi ya HR ambayo imempitisha katika safari ndefu kutoka miji mbali mbali ya Kenya.

“Nimebobea katika usimamizi wa rasilimali watu katika Chuo Kikuu cha Mt Kenya, kutoka Nairobi hadi Mombasa hadi Kisii 🤣🤣🤣 waaa imekuwa kweli,” alisema akionesha furaha yake.

Msanii huyo ambaye hajawahi ona aibu kusimulia maisha yake aliwahi nukuliwa akisema kwamba anatia bidii maishani kuwapa wanawe 5 maisha na masomo mazuri, vitu ambavyo binafsi hakubahatika kuvipata.

Akothee aliwahi nukuliwa akikiri kwamba alipata mtoto wake wa kwanza akiwa katika umri wa miaka 14 tu jambo ambalo lililemeza masomo yake lakini baadae akainukia na kuwa msanii pendwa Zaidi nchini pamoja pia na kuwa mjasiriamali aliyebobea katika biashara yake ya kampuni ya kitalii, Akothee Safaris.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved