Abigail Chams: Sijawahi fua nguo kwa mikono yangu wala sijui kupika ugali

Amesema kuwa ikiwa atatokea mchumba ambaye anataka amfulie nguo basi atamnunulia mashine ya kufua.

Muhtasari

• Chams anasema ikiwa ni lazima afanye hilo basi atafanya kwa kutumia mashine, kwani hajawahi kufanya hilo kutumia mokono yake.

Abigail Chams/Instagram
Abigail Chams/Instagram

Mcheza ala za muziki na mwanaharakati wa kijamii Abigail Chamungwana anayejulikana kwa jina la sanaa kama Chams anayetokea Kilimanjaro,Tanzania anasema kwamba hawezi kufua nguo kwa mikono yake.

Chams anasema ikiwa ni lazima afanye hilo basi atafanya kwa kutumia mashine,kwani hajawahi kufanya hilo kutumia mokono yake.

Katika mazungumzo ya moja kwa moja na kituo cha Redio cha Clouds FM, amesema kuwa ikiwa atatokea mchumba ambaye anataka amfulie nguo basi atamnunulia machine ya kufua.

“Kufua nafua kweli ila nyumbani tunatumia machine kwa hivyo siwezi kufua na mikono,lakini nadhani kwamba nikijaribu nitaweza labda.” Alisema

Aliongeza kusema kwamba;

"Ikiwa ni lazima na atasisitiza nifanye ivyo basi itanilazimu nimnunulie machine,ila naweza kujaribu kufua na mikono lakini sina uhakika kama nitaweza."

Awali  kwenye mazungumzo  na kituo hicho, Chams alisema kwamba japo ana uwezo wa kupika vywakula vingine, hawezi akapika ugali.

Mazungumzo yake yamekuwa yakiibua hisia mseto kwa mashabiki kutokana na mahojiano yake hasa pale alipokiri kwamba hajawahi  penda au kushiriki kwenye vitendo vya mapenzi

Chams mwenye umri  wa miaka 20, ni mtetezi  wa vijana kwa UNICEF nchini Tanzania ambao uathirika na afya ya kiakili na usawa wa jinsia.

Anafanya kazi sana ndani ya jamii kupitia kipindi chake cha vijana cha, `Teen Talks na Abby Chams`, ni programu  ambayo inalenga kuongeza ufahamu kwa vijana kusuhu afya ya kiakili ambayo inatenga nafasi kwa vijana kujieleza changamoto zinazowakabili na jinsi ya kukabiliana nazo.