Mtayarishaji Director Trevor, ambaye ni mchumba wa Mungai Eve,amewajibu mashabiki wake kuhusu mipango yao ya ndoa.
Trevor aliwashirikisha mashabiki wake katika kipindi cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram,huku akiwataka waulize swali lolote ambalo walihisi wanahitaji majibu kuhusu uhusiano wake na Mungai Eve.
Wakati wa kipindi hicho, shabiki mmoja alitaka kujua ni lini wawili hao wangefunga ndoa ya kuwa mume na mke.
Director Trevor aliwajibu akisema ,ingawa hawajaweke tarehe kamili ya kufunga ndoa ,wanafurahia maazimio yao ya mbeleni pamoja.
" Asante kwa kuuliza juu ya mipango yetu ya baadaye! Eve na mimi tumejitolea sana kwa kila mmoja na uhusiano wetu. Tunaamini katika kuchukua muda wa kujenga msingi thabiti wa ushirikiano wetu na kuhakikisha kuwa tuko tayari kwa hatua inayofuata. Ingawa hatuna tarehe maalum iliyowekwa kwa ajili ya harusi yetu bado, tuna furaha kuhusu matarajio yetu ya baadaye pamoja na kushiriki mpango wakati tutahisi kuwa sawa kwetu. Tunathamini usaidizi wako na uelewa wako tunapoendelea kukua na kuabiri safari yetu pamoja."
Wawili hao wamechumbiana kwa zaidi ya miaka mitano tangu Director Trevor alipomtangaza Eve hadharani kuwa mchumba wake.
Katika kipindi hicho, mashabiki walimtaka pia kutaja ni lini wanapanga kuwa na mtoto wao wa kwanza,ambapo alitaja tarehe maalum.
"Januari 26 mwaka wa 2026".Alijibu.
Aidha walitaka pia kujua nasafi yake katika Mungai Eve Media kama mwanzilishi, akisema jukumu lake ni kusimamia mwelekeo wa kimkakati.
"Kama mwanzilishi wa Cff wa Mungai Eve media online, jukumu langu linahusisha kusimamia mwelekeo wa kimkakati wa jumla wa kampuni, kusimamia ujenzi wa shughuli za kila siku na kuongoza timu yenye talanta inayokuza ushirikiano na kuhakikisha ukuaji na mafanikio ya kampuni katika dijitalii inayoendelea kubadilisha mazingira ya vyombo vya habari."
Mnamo Januari 26 mwaka huu wawili hawa walifanya sherehe ya kufana ya kusherehekea miaka mitano, muda ambao wamekaa kwenye mahusiano.