Mpenzi wa Mungai Eve, Director Trevor akiri kufuata nyayo za mmiliki wa Citizen TV

“Katika miaka mitano ijayo, nitajionea fahari kuwa mmiliki wa media kubwa nchini ya kidijitali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati," alisema.

Muhtasari

• Trevor alisema kwamba ndoto yake katika miaka mitano ijayo anajiona akiwa mmiliki wa moja ya media kubwa humu nchini.

• Trevor alifichua hili wakati wa kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram usiku wa Jumapili.

Director Trevor na Eve Mungai.
Director Trevor na Eve Mungai.
Image: Instagram

Mpenzi wa mwandishi wa habari za mitandaoni, Mungai Eve, mwelekezi Trevor amekiri kwamba mtu ambaye anamuona kama kielelezo kikubwa kwenye maisha yake na kuiga mfano wake ni mmiliki wa kampuni ya Royal Media Services, SK Macharia.

Trevor alifichua hili wakati wa kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram usiku wa Jumapili.

Alisema kwamab Mmiliki huyo wa runinga ya Citizen na stesheni zingine nyingi za redio na runinga amekuwa kielelezo chake kwa muda mrefu, tangu akiwa mdogo.

Trevor alifichua kwamba kitu kikubwa ambacho amejifunza kutoka kwa SK Macharia ni kwamba kutia bidii na kutochepuka nje ya lengo lako kuu ni njia sahihi ya kumpelekea mtu kujenga chapa yenye haiba iliyotukuka.

“Hadithi ya SK Macharia inajitokeza kama mfano hai kwamba shauku, jitihada na bidii, na uthabiti katika kile unachokifanya kunaweza kuongoza kwa mafanikio makubwa yenye historia isiyoweza kufutika,” Trevor alijibu shabiki huyo aliyetaka kujua nani kielelezo chake.

Trevor na Mungai wamekuwa waandishi wa habari za mitandaoni ambao wamevuna pakubwa kutokana na mitikasi yao na aliweza kutoa ushauri kwa wanablogu wengine ambao wangependa kuanzisha chaneli za YouTube.

“Anza pole pole na jenga ujasiri wako. Anza kwa kuunda video kwa kuzingatia maudhui ambayo unajiamini nayo. Anza na video fupi au zile za kujifunza, pole pole ongeza urefu wa video na maudhui changamano pindi unapoendelea kupata uzoefu na ujasiri,” Trevor alishauri.

Trevor alisema kwamba ndoto yake katika miaka mitano ijayo anajiona akiwa mmiliki wa moja ya media kubwa humu nchini.

“Katika miaka mitano ijayo, nitajionea fahari kuwa mmiliki wa media kubwa nchini ya kidijitali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati, kuleta mabadiliko kwa jinsi habari hutayarishwa na kupokelewa kwenye ukanda huu,” alisema kwa ujasiri.