Msanii Maandy amejibu kashfa ya kuuza mapenzi ili kupata umaarufu

Maandy amekataa madai hayo ya kujihusisha na vitendo vya mapenzi na na wandani wake hasa watayarishaji wa muziki ili kujipatia umaarufu.

Muhtasari

• Maandy amekataa madai hayo ya kujihusisha na vitendo vya mapenzi  na wandani wake hasa watayarishaji wa muziki ili kujipatia umaarufu katika tasnia ya muziki.

• Alisema kuwa, ni kawaida ya watu kulimbikizia wengine lawama, pindi wanapoona mtu anapiga hatua kimaisha.

Amanda Wambui,aka Maandy (kabaya) Instagram
Amanda Wambui,aka Maandy (kabaya) Instagram

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo  Amanda Wambui,anayetambulika kama Maandy,au kwa jina lake la utani  (Kabaya) ,amewajibu baadhi ya mashabiki wake wanao dai anajihusisha na vitendo vya mapenzi ili kupata umaarufu.

Katika mahojiano yake ya moja kwa moja na SPM BUZZ,Maandy amekataa madai hayo ya kujihusisha na vitendo vya mapenzi na  na wandani wake hasa watayarishaji wa muziki ili kujipatia umaarufu katika tasnia ya muziki.

Alisema kuwa, ni kawaida ya watu kulimbikizia wengine lawama, pindi wanapoona mtu anapiga hatua kimaisha wakidhania kwamba labda mtu hasa mwanadada hawezi kupiga hatua kwa msimamo wake mwenyewe.

Akitoa hisia zake kuhusu madai hayo alisema kuwa;

"Niliichukulia virahisi sana,ila kitambo ilikuwa ikiniuma, lakini nikaja kugungua kuwa, watu wengu hudhania kuwa wanawake hawawezi kujiendeleza bila msaada wa wanaume,au kwa bidii yao wenyewe."

Alienda mbele kusema kuwa, wanawake wengi wamelimbikiziwa lawama ya kujihusisha kimapenzi na wendani wao ili kufaulu au kujimudu kimaisha.

"Ukiangalia wanawake wengi katika tasnia ya muziki ambao wanatukanwa, ni wale ambao wameambiwa mara kwa mara kuwa pale wamefika ni kwasababu ya waume zao au wachumba wao,hivyo kwangu mimi nalichukulia virahisi kwa sababu watu wengi hawapendi kuona wanawake wakifanikiwa."

Hata hivyo alikwepa kudhibitisha ikiwa haya mambo yanafanyika katika tasnia ya muziki na kusema kwamba yeye kivyake hajaona mambo hayo yakifanyika.

"Labda yalikuwako enzi hizo, ila kwa sasa sijui maana siwezi pia nikaongelela mambo ambayo sijashuhudia. Lakini kwa sasa siwezi nikasema kama yapo."

Aidha alisema kuwa, kwa wale wanawake ambao wanafanikiwa katika shughuli zao kimaisha ni wale ambao wanafanya bidii kwa kile wanachofanya na kukipatia kipaumbele.