logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mungai Eve media imewapa kazi vijana 14 mpaka sasa - Director Trevor

Alikuwa anamjibu shabiki mmoja ambaye alitaka kupewa kazi .

image
na Radio Jambo

Makala25 September 2023 - 06:05

Muhtasari


• Akionesha tambo, Trevor aliweka wazi kwamba huwa wanapata Zaidi ya shilingi milioni 13 kutoka kwa video zao za YouTube kila wakati.

• “Ahsante lakini tayari Mungai Eve Media ina wafanyikazi 14. Miongoni mwa hawa ni videographers na wahariri,” Director Trevor alijibu.

Mpenzi wa Mungai Eve.

Mpenzi na muongozaji wa video za Mungai Eve, Director Trevor amefichua kwamba tayari wameshawaajiri vijana 14 katika kuendesha chaneli yao ya Mungai Eve.

Trevor alifichua haya wakati wa kipindi cha kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram usiku wa Jumapili.

Alikuwa anamjibu shabiki mmoja ambaye alitaka kupewa kazi nao lakini Trevor akasema kwamba mpaka sasa tayari wana wafanyikazi 14 wakiwemo wengine wa kukusanya maudhui kupitia mahojiano pamoja na wahariri wa video hizo ili kufanikisha kupakiwa kwao kabla ya muda uliowekwa.

“Ahsante lakini tayari Mungai Eve Media ina wafanyikazi 14. Miongoni mwa hawa ni videographers na wahariri,” Director Trevor alijibu.

Kijana huyo ambaye wengi wanahisi kwamba hana kazi nyingine kando na kuongoza video za mpenzi wake, aliweka bayana cheo chake katika chaneli hiyo ya pamoja.

“Mimi kama mwanzilishi mwenza wa chaneli ya Mungai Eve, wajibu wangu ni kuangalia mwelekeo wa kimkakati wa chaneli yetu, kuongoza shughuli za kila siku, kujenga na kuongoza timu ya wajuzi, kusaidi madili na kuhakikisha ukuaji wa chaneli yetu katika tasnia ya kidijitali ambayo inabadilika kwa haraka kila uchao,” Trevor alisema.

Akionesha tambo, Trevor aliweka wazi kwamba huwa wanapata Zaidi ya shilingi milioni 13 kutoka kwa video zao za YouTube kila wakati.

Hata hivyo, alisema kwamba hawana haraka ya kupata mtoto hivi karibuni na kufichua kwamba pengine mwanzoni mwa mwaka 2026 ndio wataanza kufikiria kuhusu kupata mtoto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved