logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nikuleni" Butita amjibu Georgina Njenga kumweka katika orodha ya wanaume anaowatamani

“Mimi nampenda Truekid, Butita, Manasseh Nyaga…” Njenga alisema.

image
na Radio Jambo

Habari25 September 2023 - 07:49

Muhtasari


• Aliwataja watu maarufu akiwemo mchekeshaji Eddie Butita na msanii Manasseh miongoni mwa wengine.

Georgina Njenga na Butita

Georgina Njenga amemfungia nje baba wa mtoto wake, Tyler Mbaya maarufu kama Baha Machachari katika orodha ya wanaume ambao anawamezea mate.

Njenga alikuwa akifanyiwa mahojiano na YouTuber Flossy Trukid wakati alipoulizwa kutaja wanaume wa Kenya maarufu ambao anawamezea mate.

Licha ya kuzaa na Baha mtoto mmoja na kuonesha mapenzi yao hadharani kwa Zaidi ya miaka miwili kabla ya kuachana, Georgina aliashiria kwamba muigizaji huyo hana nafasi hata kidogo kwenye moyo wake.

Aliwataja watu maarufu akiwemo mchekeshaji Eddie Butita na msanii Manasseh miongoni mwa wengine.

“Mimi nampenda Truekid, Butita, Manasseh Nyaga…” Njenga alisema.

Akimjibu katika video hiyo, Eddie Butita alitoa onyo kwa wanawake wote ambao wanakiri kwamba wanamtamani kimapenzi akisema kwamba wengi huishia tu katika kukiri hivyo lakini hawapigi hatua nyingine muhimu ya kumwambia ana kwa ana na pengine kusababisha mambo kuwa halua halua.

“Hapana!! Madem msikue mnasema tu mnanipenda na inaishia hapo, nikuleni please,” Butita alimjibu Njenga.

Awali Georgina Njenga alikiri kwamba yeye ni mke mzuri wa kuolewa lakini akasema kwamba mkwamo kidogo tu na ambao unaweza kurekebishwa na pale linapokuja suala la kuitwa kwa sherehe za wikendi.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved