Msanii maarufu duniani wa nyimbo za Bongo Diamond Platinumz, amewaombea kura wanasarakasi, Ramadhan Brothers.
Diamond Platinums,alitumia ukurasa wake wa instagram kuwapigia upato vijana hao ambao ni wacheza sarakasi wa Tanzania wanaojulikana kama Ramadhani Brothers.
Ameomba wana Afrika Mashariki wote na wale wote wanaoishi Marekani, kuwapigia vijana hao kura ili kuwawezesha kuibuka washindi wa mashindano ya Fainali America`s Got Talent ya msimu wa kumi na nane.
Katika ukurasa wake wa instagram kwenye sehemu ya stori Diamond alisema;
"Wana Afrika mashariki wote mlioko nchini Marekani,ndugu zetu @ramadhanibrothersofficial wameingia fainali katika shindano la@agt,tafadhali tuwapigie kura ili waweze kuibuka na ushindi huu wenye heshima kubwa . Kura mwisho jumanne hii, na unaweza kupiga kura zaidi ya mara kumi." Ulisoma
Kwenye mashindano hayo, wanawania kitita cha Bilioni 2.4 [shilingi za Kenya milioni 141.5],ambapo septemba 26 watashindana na zaidi ya vikundi kumi ambavyo ni pamoja na; The 82nd Aiborn Divisiona all American Chorus,Avantgardey,Chibi unity,Anna Degzman,Putti Ariani,The Msanzi Youth Choir, Murmuration,Ahren Belisle,Lavender Darcangelo,na Adrian Stoica pamoja na Hurricane katika Fainali hiyo.
Vijana hawa wa Ramadhani Brothers ambao wanatokea Tanzania, uburudisha kwa kutumia sarakasi.
Ndugu hawa wanatumia mchanganyiko wa mizani yenye nguvu ya juu sana kwa kutumia mikono ,kuwekeleana kichwa na mambo mengine ya ajabu ambayo uishia kuwaacha watazamaji na mshangao mkubwa.