logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jimal Rohosafi amefichua kufanya upandikizaji wa nywele kwa miaka 6 sasa

“Muda wote jipende kwanza,” Jimal alisema.

image
na Radio Jambo

Habari26 September 2023 - 04:19

Muhtasari


• “Amira si alisema alifanya transplant akakana aty ni hair growth oil😂😂aaah shosho media,” Glam by Chibby alisema.

Jimal Rohosafi.

Mjasiriamali Jimal Rohosafi amezua gumzo mitandaoni baada ya kufichua kwamba nywele ambazo mashabiki wake wamekuwa wakimuona nazo kwa karibia miaka sita sasa si za kiasili bali ni za kupandikiza.

Mfanyibiashara huyo alifichua haya kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alipakia msururu wa picha na video akikutana na daktari ambaye amekuwa akimpa huduma hiyo nchini Uturuki kwa muda sasa.

Rohosafi alisema kwamba hii ni mara ya pili alikwenda Uturuki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza nywele na kudai kwamba daktari wake alisema hivi karibuni ataleta huduma hizo Kenya ili kutoa suluhu kwa watu ambao wamekuwa na changamoto ya kupotea kwa nywele.

“Muda wote jipende kwanza,” Jimal alisema katika picha moja aliyopakia akionesha jinsi alifanyiwa ufundi wa kupandikiza nywele feki kichwani.

“Huyu ni daktari wangu kwa miaka 6 iliyopita hatujawahi kutana lakini sasa tumekutana tena. Kuna mambo mengi yualiyokuwa yakiendelea wakati wa Covid-19 na sikuweza kurudi hapa kufanya upandikizaji wangu wa pili wa nywele bandia lakini sasa nimerudi kufanya upandikizaji wa nywele kutoka kwa daktari mahiri duniani wa kupandikiza nywele,” alisema.

Jimal alipakia msururu wa video wakitembea na daktari huyo wake na pia wakiwa ndani ya gari na kudokeza kwamba alikuwa anaendea awamu ya pili na ya mwisho katika mchakato mzima wa kupandikiza nywele bandia kichwani.

Baadhi ya mashabiki wake walimsuta kwenye upande wa kutoa maoni wengine wakikumbuka maneno ya aliyekuwa mke wake Amira kwamba huwa anafanya upandikizaji wa nywele bandia kichwani lakini mashabiki hawakuamini hadi mwenyewe amejisemea sasa.

“Amira si alisema alifanya transplant akakana aty ni hair growth oil😂😂aaah shosho media,” Glam by Chibby alisema.

“Kumbe Amira was saying the truth😂” Sumei.a aliandika.

“Lakini si ulisema Amira ameenda turkey surgery so Na wewe ulienda kupandwa nywele 10/10” Imman Ffay alimuuliza.

“Kumbe Amira said the truth ulienda Turkey kupanda nywele kuficha kipara 😂😂😂” Kerry Maccambie aliradidi.

“Kumbe ulichongoa mama watoto alienda Turkey surgery kumbe pia wewe 😂😂😂😂” Tbaby721.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved