logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Marioo anusurika ajali ya ndege wakiwa angani Afrika Kusini

“Ghafla ndege ikaanza kuyumba sijui ndio ilipita kwenye mawingu." Marioo.

image
na Radio Jambo

Habari26 September 2023 - 07:05

Muhtasari


• Kwa hali ya kuogofya, Marioo alisema kwamba ndege ilizidi kuyumbishwa Zaidi na alichokiwaza na kukiona katika fikira zake ni mwisho wake duniani.

• "Na kilichonichanganya Zaidi ni baada ya kuona wale wahudumu wenyewe ni kama hawaelewi hivi kama wamechanganyikiwa,” Marioo alihadithia.

Marioo.

Msanii Marioo amesimulia uzoefu ambao hakuna mtu aliye hai anaweza kuutamani.

Msanii huyo ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akionesha mashabiki wake jinsi wamekuwa wakila bata Afrika Kusini akiwa na watu wake wa karibu akiwemo meneja na produsa wake Abbah.

Msanii huyo sasa amesimulia kwa uchungu jinsi walinusurika ajali ya ndege wakiwa angali na hata kupakia video ambayo walirekodi jinsi ndege ilivyokuwa ikiyumba kila mmoja akishikilia roho yake.

“Basi leo asubuhi tulikuwa tunatoka zetu Johannesburg tukienda mji mwingine, aisee usiombe hiki kitu kisikukute, ndege imepaa tu vizuri ilivyofika angani ikaanza kupiga hizo kelele. Ndege ilivyozidi kwenda juu Zaidi ndio hizo kelele zikaongezeka kiasi kwamba hata huyo rubani akiongea hamsikii kabisa. Na kilichonichanganya Zaidi ni baada ya kuona wale wahudumu wenyewe ni kama hawaelewi hivi kama wamechanganyikiwa,” Marioo alihadithia.

Kwa hali ya kuogofya, Marioo alisema kwamba ndege ilizidi kuyumbishwa Zaidi na alichokiwaza na kukiona katika fikira zake ni mwisho wake duniani.

“Ghafla ndege ikaanza kuyumba sijui ndio ilipita kwenye mawingu. Japo ndege kutingishwa na upepo au mawingu ni jambo la kawaida ila kwa sababu ya zile kelele ndio nikazidi kuona mwisho ndio umefika,” alisema.

Hata hivyo, msanii huyo wa Mama Amina alishukuru Mungu kwa kutua salama na kusema kwamba huo ndio ulikuwa uzoefu mbaya amewahi kuushuhudia akiwa kwenye safari ya ndege.

“Imagine Ndege imepiga kelele kwa saa 2, imeyumba 45 nzima. Hapo nawaza naona ni kama Mungu ananiuliza ‘Eeeh unasemaje sasa! kimoyo moyo nasema ‘mzee sina ujanja fanya vile unavyoweza’… ila tunamshukuru Mungu tulifika salama lakini imebidi nilale masaa 6 ndio niweze kusikia vizuri,” alimaliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved