Fahamu kwa nini Aslay anatumia simu ya kaduda licha ya kuwa msanii mkubwa kwa miaka

Aslay alisema starehe yake huishia kwa kucheza michezo ya PS4 tu wala sio kama wengine wanaotumia muda mwingi katika kubonyeza vitufe kwenye simu.

Muhtasari

• Aslay alisema kwamba kama kuna kitu kinaweza kikamharibia siku yake yote na kumchukua mtu ni kutukanwa na mamake.

Aslay afunguka kwa nini hawezi imba Amapiano.
Aslay afunguka kwa nini hawezi imba Amapiano.
Image: Instagram

Msanii Aslay amewashangaza wengi baada ya kufichua kwamba licha ya kuwa na simu ya kisasa aina ya kishkwambi, yeye anapendelea sana kutumia simu ndogo ya mulika mwizi, Wakenya wanasema ‘Kaduda’.

Msanii huyo aliwashangaza watangazaji kwenye mahojiano walipomuuliza tetesi kwamba huwa hapatikani kwa urahisi pengine kutokana na ugumu wa kimawasiliano wakimtaka kufichua kama kweli ana simu nzuri ya kisasa.

Aslay alisema kwamba ni kweli ana simu nzuri yena ya kisasa ambayo anatumia kwenye kuendeleza maisha yake ya mitandaoni lakini akasema kwamba mazingira ambayo amekulia yamemsababishia kutopenda kutumia simu hizo sana huku akikiri kwamba ana kasimu kadogo ‘kaduda’.

“Ndio yale maisha niliyozoea ya kuishi ndani ndani kiasi kwamba yashanikuza mpaka nimeona kila siku niko vile vile. Nimeyazoea mpaka nimezoea lakini simu natumia kila siku na ukitaka kunitafuta utanipata tu. Sio hii simu ya smartphone, ni simu cha kitochi tu vizuri nakitumia,” Aslay alisema.

“Smartphone ninayo lakini sijui niseme ndio mazoea lakini sasa hivi si mnaona niko freshi naposti nafanya nini,” aliongeza.

Msanii huyo pia aliwashangaza wengi kwa kusema kwamba licha ya kupenda kuwa na simu lakini muda mwingine anaweza akakaa hata siku nzima bila kugusa simu yake na wala hana wasiwasi wowote kuhusu watu watakaomtafuta.

“Napenda, si mnajua simu ndio kila kitu lakini sio kila wakati nikae na simu. Presha ya simu mimi siwezi kuimudu, naweza nikakaa hata siku moja nzima,” alisema.

Aslay alisema starehe yake huishia kwa kucheza michezo ya PS4 tu wala sio kama wengine wanaotumia muda mwingi katika kubonyeza vitufe kwenye simu wakihama kutoka mtandao mmoja hadi mwingine.

Aslay alisema kwamba kama kuna kitu kinaweza kikamharibia siku yake yote na kumchukua mtu ni kutukanwa na mamake.

“Mimi vitu ambavyo vinanipa hasira haraka na kupotexza moods zangu, mimi naeza nikasema kwanza kutukanwa na mamangu, ukinitukania mamangu na ukijua kabisa mamangu haayuko sehemu Fulani, hicho kinaweza kuniharibia siku nzima,” alisema.