Mkewe marehemu Mowzey Radio afukuzwa kwenye nyumba kisa deni la rent ya miezi 18

Mjane huyo anadaiwa zaidi ya shilingi milioni moja za Kenya kama malimbikizi ya kodi ya nyumba hiyo ya kupanga kwa miezi 18.

Muhtasari

• Hata hivyo, kutokana na sababu ambazo bado hazijajulikana, tangu Aprili 2022, Lilian Mbabazi hajatii suala la kulipa kodi yake.

• Hii ilimlazimu mwenye nyumba kuhusisha mamlaka, na mawakili wake walitoa notisi ya madai kwa Lilian Mbabazi.

Mjane wa Mowzey Radio, Lilian Mbabazi.
Mjane wa Mowzey Radio, Lilian Mbabazi.
Image: Instagram

Mjane na mwimbaji marehemu Mowzey Radio kutoka nchini Uganda, Lilian Mbabazi yuko kwenye hatari ya kufukuzwa kutoka kwa ukodishaji wake kwa kushindwa kulipa malimbikizo yake ya kukodisha, vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bw. Sitran Deshpande, ambaye ni mwenye nyumba wa Lilian Mbabazi, mwimbaji huyo alikodisha nyumba hiyo tangu 21 Februari 2018 kwa kila mwezi Ugx 1.5M [Shilingi za Kenya elfu 59].

Hata hivyo, kutokana na sababu ambazo bado hazijajulikana, tangu Aprili 2022, Lilian Mbabazi hajatii suala la kulipa kodi yake.

Hii ilimlazimu mwenye nyumba kuhusisha mamlaka, na mawakili wake walitoa notisi ya madai kwa Lilian Mbabazi.

Wakili Sufian aliongeza kuwa licha ya kupata notisi hiyo ya madai, Lilian amekuwa akicheza kujificha akidai jinsi ambavyo amekuwa akipita na kurudi mjini hivyo kuwa vigumu kwake kutimiza ahadi zake.

Alibainisha zaidi kuwa pamoja na kwamba Lilian alidai kuwa bado ni mpangaji, aliacha mali zake zote kimya kimya; hata hivyo, mwimbaji huyo alikanusha hili wakati alipopigiwa simu na kushikilia kuwa alikuwa anatazamia kukutana na wahusika siku ya Alhamisi.

Lilian alizidi kudokeza kuwa amekuwa akitarajia pesa za kulipia kodi anayostahili kulipa, lakini jambo hilo limecheleweshwa.

Sufian alimtaka Lilian bila kukosa kujitokeza katika Kituo cha Polisi Konge siku ya Alhamisi, ili aweze kufungua nyumba kwa mamlaka kuchukua hatua.

Mowzey Radio, aliyejulikana kutoka kwa muziki wake na msanii mwenza Weasel, alifariki Februari mwaka 2018 baada ya mabishano na baunsa wa klabu moja jijini Kampala ambaye alisemekana kumdunda sakafuni na kufariki.