Kiongozi wa kidini adai anaweza kumfufua Mohbad iwapo ataruhusiwa kuona maiti yake

Kiongozi huyo mwenye mashurubu si haba alionekana amevalia vazi jeupe akirekodi video kwenye chumba chake akizitaka mamlaka kurahisisha kazi kwa kumruhusu kuona maiti hiyo kisha kuifufua.

Muhtasari

• Kiongozi huyo wa dini alikuwa anazungumza kwa lugha isiyo rasmi ya kabila moja la huko Nigeria alionekana akiwa kwenye nyumba yake akirekodi video hiyo.

Mtu ajitokeza akidai kuwa na uwezo wa kumfufua Mohbad.
Mtu ajitokeza akidai kuwa na uwezo wa kumfufua Mohbad.
Image: Insta

Huku kifo cha msanii Mohbad nchini Nigeria kikiwa tayari kimevutia dhana tofauti tofauti, sasa kiongozi mmoja wa kidini ameibuka kwenye video akikiri kwamba ana uwezo wa kumfufua iwapo atapatiwa nafasi ya kuona maiti yake.

Katika video ambayo imesambaa, kiongozi huyo wa kidini aliyetambulika na blogu za Nigeria kama Oba Ewulomi alidai kwamba anaweza kumfufua Mohbad ikiwa atapewa ufikiaji wa maiti ya mwimbaji huyo.

Kiongozi huyo wa dini alikuwa anazungumza kwa lugha isiyo rasmi ya kabila moja la huko Nigeria alionekana akiwa kwenye nyumba yake akirekodi video hiyo.

Kwa muonekano, anakaa kama kiongozi wa dini ya Kiislamu kutokana na masharubu yake na gauni jeupe kama Waislamu, alinukuliwa akisema kwamba anachokihitaji ili kumfufua Mohbad nit u kupewa idhini ya kuufikia mwili wake ambao ulifukuliwa mwishoni mwa wiki jana.

Madai ya Oba Ewulomi yanakuja kufuatia kifo cha Mohbad mnamo Septemba 12 na baadaye kufukuliwa kwa mwili wake kwa uchunguzi mnamo Septemba 21.

Ni muhimu kutambua kwamba madai kama hayo ya ufufuo mara nyingi yanatiliwa shaka na yanapaswa kuchunguzwa na uchunguzi wa kisayansi.

Katika visa vya vifo visivyotarajiwa, uchunguzi wa maiti hufanywa ili kubaini sababu ya kifo, na wataalamu wa matibabu hutegemea kanuni zilizowekwa za kisayansi kufikia hitimisho lao.

Kuheshimu maiti na matakwa ya familia zao ni muhimu sana wakati wa uchunguzi kama huo, na madai ya nguvu zisizo za asili yanapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari na kutilia shaka hadi yathibitishwe kupitia njia zinazofaa, mtumizi mmoja wa mitandao aliyekashfu vikali dai hilo la ufufuo aliandika.