Ramadhani Brothers lamaliza nafasi ya 5 kwenye mashindano ya AGT

Kupitia ukurasa wao wa Instagramu, wamekubali matokeo na kuwapongeza mashabiki kwa kusimama na wao kwa kuwapigia kura.

Muhtasari

•Ramadhani Brothers walibwagwa na jamaa  anayetambulika kama Adrian Stoica na mbwa wake Hurricane na kuondoka na kitita cha pesa  dola milioni moja ambazo ni sawa na Sh 147.7 milioni za Kenya.

Ramadhani Brothers/Instagram
Ramadhani Brothers/Instagram

Kundi la sarakasi kutoka nchini Tanzania, Ramadhani Brothers, limekamata bafasi ya tano katika Fainali za mashindano ya America`s Got Talent.

Vijana hao walifaulu kuingia katika fainali za mchuano  wa kuigiza kwa njia ya sarakasi na hivyo majibu yalipotoka wakakamata nafasi ya tano.

Ramadhani Brothers walibwagwa na jamaa  anayetambulika kama Adrian Stoica na mbwa wake Hurricane na kuondoka na kitita cha pesa  dola milioni moja ambazo ni sawa na Sh 147.7 milioni za Kenya.

Kupitia ukurasa wao wa Instagramu, wamekubali matokeo na kuwapongeza mashabiki kwa kusimama na wao kwa kuwapigia kura.

"Jamani,matokeo yametoka,hatukukusanya kura za kutosha, hivyo tumeshika nafasi ya 5kwenye kinyanganyiro hicho. Tunataka kushukuru America`s Got Talent kwa nafasi hiyo na watu wote waliotupigia kura. Mapambano yanaendelea." Walisema.

Mashabiki waliokuwa wakifuatilia sarakasi ya vijana hao,wamewapongeza kwa kazi njuzi na kuwapa moyo kama alivyo andika mtumiaji mmoja wa mtandao huo akisema,

"America`s Got Talent sio kuwa mshindi,ila inahusu kujenga jina na mmefanya hivyo kwa kuingia katika fainali na sio fainali tu bali kutokea kwa nafasi ya tano. Hongera brothers."

Awali kabla ya mashindano hayo kuanza, Msanii Diamond alikuwa amewapigia upato kwa kuwaombea kura kwa watu wote Afrika wakiwemo wale ambao wanaishi ngambo.

Diamond aliandika kwenye kurasa wake wa Instagramu kwenye stori,akiwapongeza vijana hao kwa kuwahi kufika Fainali.

Ramadhani Brothers, sasa wamesema  kuwa safari bado na kuahidi kuendelea na mazoezi yao mara kwa mara, ili kujiweka tayari kwa lolote.