Vanessa Mdee na Rotimi washerehekea mwanao wa kiume kufikisha miaka 2

Vanessa Mdee na mumewe Rotimi awakuweza kuficha furaha yao kwa mwanao kufikisha miaka mbili

Muhtasari

• Muigizaji  na mwimbaji wa Tanzania walimkaribisha mtoto wao Seven Adeoluwa Akinosho mnamo 2021.

Vanessa Mdee na mchumba wake Rotimi wako kwenye likizo ya familia kusherekea kuzaliwa kwa mwanaowao wa kwanza wa kiume anayejulikana kwa jina Seven anatimiza miaka miwili.

 Alitangaza furaha yake kwa mtoto wake kutimiza miaka miwili,"Hapa ni kufanya kumbukumbu," Vanessa alinukuu video kwenye uwanja wa ndege mnamo Septemba 26, tayari kwa kupanda ndege.

Baadaye, video nyingine inamwonyesha Rotimi akiwa katika eneo lao, kwenye kidimbwi cha kuogelea na mtoto wao  Imani Enioluwa.

Tukio la kupendeza na Imani lilimgusa sana Vanessa hivi kwamba aliongeza furaha usoni ili kuonyesha upendo wake kwa kuona jinsi baba Rotimi alivyo mzuri kwa watoto wao.

Muigizaji  na mwimbaji wa Tanzania walimkaribisha mtoto wao Seven Adeoluwa Akinosho mnamo 2021.

Wanandoa hao walishiriki picha za karibu na mtoto wao mchanga kwenye akaunti zao na kufichua jina lake pamoja na emoji za taji na hua kwenye nukuu.

 "Tuna furaha kubwa kumkaribisha mwana wetu,kama wazazi wa mara ya kwanza, kila kitu kuhusu tukio hili kimekuwa changamoto mpya kabisa".Vanessa alisema

Kila mmoja wao alieleza aina ya mzazi ambaye angekuwa,Rotimi aliliambia Jarida la People kuwa yeye ni "mama mwenye shauku, upendo na ulinzi.

Mdee kwa upande wake, alimsifu Rotimi akisema amekuwa  baba mtulivu,  mkusanyaji na mwenye furaha ambaye pia ni mwalimu mzuri wa nidhamu katika mawasiliano.

Wawili hao walichumbiana mnamo 2020 Disemba huko Atlanta baada ya kukutana kwenye Tamasha la Essence baada ya karamu.