Mwimbaji Otile brown amewaandikia ujumbe wafuasi wake kwenye Instargam akiwataka siku zote wazidi kuomba na kufanya mema ila wasidhani mungu amewasahau.
Kupitia ukurasa wake Otile amefichua jambo ambalo amesema kwamba watu wengi wana wivu na majigambo jambo ambalo huwafanya kupitwa na baraka zao kila wakati Otile akifichua haya kwa watu wote wanaomuunga mkono katika sanaa yake ya muziki.
"Mungu alishatubariki zamani ila tunazipitaga njiani kila siku mana tunaedeshwa na wivu chuki na majigambo".....Mwimbaji huyu aliendelea na ujumbe wake akisimulia zaidi alihomaanisha kwa wafuasi wake.
"Ninacho maanisha ni kwamba wakati mwingine yule unayetaka sana kumshusha huenda yeye ndio njia pekee ya mafanikio yako ". alisema mwimbaji huyu.
Otile brown kwa kumalinzia ujumbe wake aliweza kufafanua kuwepo kwa baraka za mungu katika maisha ya mwanadamu.
"Baraka zinakuja kwa njia tofauti,baraka zetu huenda zikapatikana ata kwa adui ila tunapokosa busara na unyenyekevu tutazindi kudhania kua mungu alitusahau ,wakati wote mafanikio yanaanza akilini ".Otile alisema