Wema Sepetu - sikutaka kukosana na mpenzi wangu ndio maana niliacha ulevi

Mwigizaji nchini Tanzania asimulia maisha yake baada ya kuacha vileo

Muhtasari

• Wema kwa miaka mingi amejihusisha na uingizaji wa filamu na kujizolea zawadi chungu nzima. 

 

Wema Sepetu azungumzia kuhusu mafanikio ya maisha yake
Wema Sepetu azungumzia kuhusu mafanikio ya maisha yake
Image: Instagram, Matkaba

Mwigizaji mwenye wa filamu za Bongo  mwenye uzoefu Wema Abraham Sepetu amefunguka kuwa ana takribani  mwaka tangu aache kutumia vileo vya aina yoyote.

 Wema hakuficha furaha yake wakati wa kusherekea siku yake ya kuzaliwa baadaa ya waingizaji na wasanii maarufu kumtembelea.

Sherehe hii na ambayo ilifanyika nyumbani kwa muigizaji huyu ilihudhuriwa na wasanii wengi akiwemo Hamisa Mobbeto,Nandy,na Ruby.

Wema kwa miaka mingi amejihusisha na uingizaji wa filamu na kujizolea zawadi ghali. Aliongeza kuwa kwake siku ya kuzaliwa ndio siku muhimu sana maishani mwake.

 

'Nina furaha sana leo wengi wanashindwa kwa nini nimefanya sherehe ghali mna lakini kwangu mimi siku hii ni muhimu kuliko siku zote nimebarikiwa sana na wakati mtu anapozidi kuwa na umri mkubwa ndipo ana uwezo wa kusherekea zaidi"..

Muigizaji huyu alipozidi kuhojiwa na wanablogu alisimulia zaidi  cha muhimu kwa baada ya kukaa miezi kadhaa bila kutumia vileo.

"Kwa hakika watu  wengi akiwemo mamangu mzazi na mpenzi wangu walitaka niache pombe kwa muda mrefu jambo ambalo nafurahi sana kwa kweli najuta maisha niliokuwa nayo wakati nitumia pombe ila kwa sasa moyo wangu umejawa na amani kwa kuacha pombe .

Mara mingi tungetofautiana na mpenzi wangu kwa tabia zangu za pombe kwa niliona jambo hili linaweza kuleta mfurugano kwa kuwa mume wangu hapendi ulevi.

Wema alimsifu mumewe na marafiki kwa kufanikisha kwa kugharamikia vyakula na hata mapambo ya sehumu iliyotengwa kusherekea siku yake ya kuzaliwa.