Staa wa bongo Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny ni msanii mwenye huzuni baada ya jukwaa la bwawa la maji alilokuwa amejenga kuporomoka baada ya kujazwa maji.
Bosi huyo wa lebo ya Next Level Music alikuwa amepanga kuwatumbuiza mashabiki wake katika mkoa wake wa nyumbani, Mbeya akiwa amepanda boti ndani ya bwawa lililojengwa uwanjani lakini ndoto hiyo yake ilikatizwa baada ya bwawa hilo kuporomoka.
Katika taarifa ya kusikitisha Jumapili asubuhi, msanii huyo wa zamani wa WCB alifichua kuwa alitumia zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania (Ksh 4M) kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo na hata alitafuta huduma za wahandisi bora ili kufanikisha ndoto yake.
“Hii show niliokua nimepanga na team Yangu ilikua ni show ya ndoto yangu nimeiota kwa muda mrefu sana yani ( Kuweka maji na kuingia na Boat) lakini sehemu ya uwanja wa show Ilikua ndoto yangu kufanya show ya tofauti nyumbani kwangu , Ambayo muda huu nilikubali kutumia kiasi. kikubwa sana cha pesa kivyovyote vile ili nifanikishe, Hua ninapofanya wazo kwa umakini mkubwa sana ndio hua tunautanguliza mbele yani licha ya kutafuta ma Engineer na watu waliobobea kwenye sekta ya matengenezo ila PLAN YANGU YOOTE HAIKUFANIKIWA ���������,” Rayvanny alisema kupitia Instagram.
Aliambatanisha maelezo yake na video inayoonyesha ujenzi wa bwawa hilo tangu mwanzo hadi karibu kukamilika kisha kuporomoka.
Kulingana na video hiyo, bwawa lilikuwa tayari limekamilika na boti ambayo Rayvanny angetumbuizandani yake ilikuwa imeagizwa na ilikuwa ikisubiri kufanyiwa majaribio kwenye bwawa hilo wakati tukio la bahati mbaya lilipotokea. Mwimbaji huyo alidokeza kulikuwa na mchezo mbaya kwenye tukio hilo kwani alishuku kuwa kuna mtu ambaye alitoboa shimo kwenye bwawa hilo na kufanya ukuta kuwa dhaifu.
“Team na mimi wote tuliingiwa na majonzi makubwa sana ikabidi nianze kuwafariji hadi hakija aliandika kitu wakati ukweli ni mambo ambayo yalitangaza kuwaambia wakuu, kwamba taarifa na kujiridhisha kua kazi imekamilika nikapata kazi ya kutafuta maana swala letu lilikamilika na tukawa tunasubiri ya boat. ila watu wasio kua na nia njema pia waliweza kulikamilisha jaribio hilo Maana Upande uliod ulitobolewa mashimo chini kipindi hiki tuko busy na matengenezo mengine ya Idea yetu!!! ," alisema.
Hata hivyo alidokeza kuwa tayari amejifunza kukubali changamoto zinapokuja kwani damia zitakuwa sehemu ya maisha.