Mchekeshaji wa muda mrefu ambaye pia aliwania kiti cha ugombea wa ubunge South Imenti, MC Jessy ,amefichua kuwa kuwania kiti chochote cha siasa ni gharama mno kwa anayegombea.
Baada ya mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu mchekeshaji huyu alisimulia jinsi ambavyo mambo yalikuwa wakati wa siasa za mwaka wa 2022 licha ya kuwa alipoteza kiti hicho.
"Nilikuwa nashidana na jamaa wa miaka 71 mwanaume ambaye alikuwa amejaribu kuwania kiti hiki kwa mihula minne mbila kufanikiwa kwa kweli kiti hicho kilinigharimu zaidi ya millioni 58,South Imenti ina maeneo mengi jambo ambalo ilitulazimu tuwe na gari 12 ...
Kila gari ilizunguka kunipigia debe kutoka asubuhi hadi jioni bei ya mafuta ilikuwa ghali mno kila gari ilikuwa na mtangazaji ambaye angeuza sera zanguka kwa wenyeji, wote walikuwa wanataka mshaara wao jioni kwa siku tungetumia zaidi za laki mia tatu". Mc Jessy alisema.
Mc Jessy alisema kwamba kwa siku magari yake pamoja na wasaindizi wake akiwemo meneja wake wa uchanguzi wangetumia zaidi ya elfu 50 kwa kila gari wakati ambapo wangefika maeneo ya kuunza sera zao kwa wakaaji wa maeneo mbunge ya South Imenti.
Mchekeshaji huyu pia alizungumizia mgombea wa ubunge Mathare ,Bahati akikiri kuwa yeye ndiye aliyemtambulisha kwa chama cha UDA ,Bahati alisimulia pia alitumia zaida ya millioni 27 kuwania kiti cha ubunge Mathare licha ya wote kupoteza .