Aslay asimulia kilichomgusa kuwapa wanawake Kanga siku ya maadhimisho ya miaka 10 ya mziki

Nawaheshimu sana wanawake ndipo niliamua kuwapa kanga kwa heshima ya mamangu aliyetangulia

Muhtasari

•Tulishirikiana pamoja na timu yangu kwenye siku yangu ya kusherekea miaka kumi kwenye muziki tuwape wanawake kanga ili kukumbuka mamangu na kumpa heshima yangu  ndipo niliamua kuwapa kanga wanawake

Aslay
Aslay
Image: Instagram

Msanii  maarufu  nchini Tanzania wa nyimbo za Bongo Aslay, jina lake kamili Aslay Isihaka Nassoro, siku chache baada ya kuaandaa sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka kumi kwenye muziki ametangaza kwa nini aliamua kuwapa wanawake zawadi.

Licha ya kuwa mamake mzazi alifariki akiwa mdogo sana wakati alipokuwa anachipuka kwenye  muziki Aslay alisimulia kuwanza sana jambo hilo akikumbuka upendo wa mama na jinsi alivyokuwa hodari kwa kuzitengeneza kanga.

 "Niliamua kuleta kubukumbu ya mama kwa karibu nami jinsi mama alivyopenda kanga nilipatwa na wazo na kushirikiana pamoja na timu yangu katika siku yangu ya kusherekea miaka kumi kwenye muziki tuwape wanawake kanga ili kukumbuka mamangu na kumpa heshima yangu  ndipo niliamua kuwapa kanga wanawake kwa ".Alisema aslay.

Aslay alisimulia jinsi alivyompenda mamake akisimulia kwamba alimjengea mamake nyumba akiwa na umri wa miaka kumi na tatu wakati nyota yake ya muziki ilichipuka.

Huku akiwa kwa mahojiano na wanahabari Msanii huyu wa Bongo alisimulia jinsi ambavyo amejitahidi huku akiwatangazia wafuasi wake kwamba yupo tayari kuwapa burudani mpya akiwa anashirikiana na timu yake.