Msanii maarufu wa Bongo nchini Tanzania Diamond kupitia mtandao wake wa instagram amedhihirisha wazi upendo wake kwa mwanaye Naseeb Juniour kwa maneno matamu akimsifu baada ya picha za pamoja wakisherekea siku yao ya kuzaliwa.
Tarehe mbili mwezi wa Octoba kila mwaka kwenye kauli aliyotangaza Diamond ni siku muhimu sana maishani mwake ikiwa ni siku ambayo yeye na mwanawe husherehekea pamoja siku yao ya kuzaliwa .
"Kusheherekea siku ya kuzaliwa siku moja na mwanangu ni furaha tele maishani mwangu ,najivunia kuwa nawe Naseeb Junior kwangu ni heshima na baraka mingi ,nakupenda sana mfalme wangu".Alisema Diamond kupitia mtandao wake.
Diamond kupitia mitandao ya kijamii aziweka picha walizopigwa pamoja na mwanawe akifurahi jinsi amekuwa mkubwa kupitia mtandao mamake msanii huyu wa Bongo alizungumzia jambo ili akitanja kuwa damu ni zito kuliko maji baada ya kuona wawili hawa pamoja.
Naseeb Juniour ni mtoto wa kiume wake msanii Diamond Platnumz's ambaye walifanikiwa kumpata na aliyekuwa mpenzi wake mkenya Tanasha Donnah.