logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbunge Peter Salasya aeleza aina ya mwanamke anayetaka kumuoa

Zaidi Peter Salasya amefichua sababu inayomfanya asitumie gari lake la V8 siku hizi.

image
na Radio Jambo

Burudani07 October 2023 - 09:02

Muhtasari


  • Peter Salasya alishiriki safari yake ya kisiasa na kwa nini anahisi kuwa yeye ni mmoja wa wabunge waliofanikiwa hadi sasa ambao wamepata Kitu.
Mbunge Salasya azungumza sababu za kutonyoa nywele

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya alizaua hisaia mseto mitanadaoni akiwa kweanye mahojiano siku ya ijumaa.

Peter Salasya alishiriki safari yake ya kisiasa na kwa nini anahisi kuwa yeye ni mmoja wa wabunge waliofanikiwa hadi sasa ambao wamepata Kitu.

Kulingana na Peter Salasya kuwa mbunge haikuwa safari rahisi. Hii ni kwa sababu anapokumbuka mara ya kwanza aliposhiriki uchaguzi mwaka 2017 alikuwa wa mwisho kwa kura 254 kutoka eneo bunge lake.

Zaidi Peter Salasya amefichua sababu inayomfanya asitumie gari lake la V8 siku hizi.

Kulingana na Peter Salasya ni kwamba haendeshi gari lake kwa sababu ya gharama ya mafuta ya petroli.

Alisema kuwa gari lake hutumia mafuta mengi ikilinganishwa na magari mengine. Na gharama ya mafuta ya petroli ilipopanda aliamua kuegesha gari lake kwani sasa alikuwa akinunua mafuta maradufu.

Peter Salasya alifichua kilichomfanya kuwa mbunge na kwanini amechagua kuwa tofauti na wabunge wengine wanaokaa Bungeni.

Zaidi ya hayo, Peter Salasya alifichua sababu kwa nini bado hajaoa. Kulingana na Salasya ni kwamba aliachana na uhusiano hii ni kwa sababu alipokuwa bado raia wa kawaida kabla ya kuwa mbunge hakuna mwanamke aliyemtaka tangu alipoachana.

Peter Salasya aliongeza kwa kusema kuwa ndoto yake ni kuoa mrembo wa kizungu kutoka mataifa mengine nje ya Afrika.

Hii ni kwa sababu kwake anahisi kuwa ni wanawake weupe tu ndio wangeelewa kwa urahisi kuhama kwake na kile anachotaka ikilinganishwa na wanawake wa Kiafrika.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved