Msanii wa Bongo Flava nchini Diamond Platnumz amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Samia Suluhu kwa kuwa anaongoza nchi katika hali ya msukosuko wa kiuchumi.
Akizungumza mjini Iringa ,Tanzania kabla ya tamasha lake, Diamond alieleza kuwa mama Samia Suluhu ni Rais anayetahili kupewa nafasi ya kuongoza nchi.
Diamond ambaye alionekana kuunga mkono uongozi wake pia alipinga upinzani akisema wanafanya kama vikwazo kwa kueneza taarifa za uongo kuhusu uongozi wake.
"Ni mara ya kwanza kuwa na Rais ambaye ni mwanamke. Ikiwa mama zetu wangeweza kutuongoza,yeye angeshindwa vipi? Lakini wako wanaotaka kuwa kikwazo anapotumia uongozi wake. Hata hivyo wanaume kama sisi tuliolelewa na single Mothers inabidi tuungane na tuungane nyuma yake kwani anaongoz." Alisema
Alitoa changamoto kwa kila aliyekuwapo kumpa heshima na upendo Rais suluhu kama walivyowafanya mama zao wazazi.
"Kama unampenda na kumheshimu mama yako aliyekulea hadi hapo ulipo basi amini kuwa Rais ambaye kwa sasa yuko kitini anaweza kutuongoza vyema. Hata wakati amabpo raia wengine wanapoinuku dhidi yake kueneza hadithi mbaya na za uongo,lazima tujitokeze.Hii ni mra ya kwanza tuna kiongozi wa kike anayewakilisha. Basi usiwasikilize wabadhirifu wanaotaka kumharibia sifa yake."
Kati ya mwezi wa Septemba,kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais Tundu Lissu wlikuwa wamekamatw kwa madai ya mkusanyiko usio halali.
Lissu,makamu mwnyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania amekuwa aifanya mikutano ya kisiasa nchini humo tangu aliporejea kutoka uhamishoni mwezi Januari,akiukosoa utawala wa Rais Suluhu kwa Rekodi yake ya haki za binadamu.
Ingawa aliachiliwa kwa dhamana,Lissu bado ni mkosoaji mkali wa utawala unaoongozwa na Suluhu.