logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Karen Nyamu ajibu shutuma za Pasta T kuhusu zawadi yake ya pombe kwa Samidoh

Haya yanjiri siku chache baada ya Pasta T kuwakosoa wanasiasa ambao wanaenjoi maisha huku rai wakihangaika na hali ngumu ya maisha.

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 October 2023 - 11:09

Muhtasari


  • •Pasta T,alionyesha kutoridhika wakati amabapo mwanasiasa anatumia takriban sh 420,000 kwa pombe,hisia ambazo zilionekana kumlenga Karen Nyamu.
Karen Nyamu na Pasta T.

Karen Nyamu,amejibu shutuma kutoka kwa Pasta T kuhusu zawadi yake ya pombe yenye thamani ya zaidi ya sh.420,000 kwa Samidoh.

Akishiriki video ya mahubiri ya Pasta T,Karen alihoji ni kwa nini mchungaji huyo anapendelea noti mpya ya pesa na kusema kwamba Mungu ataki pesa akitaka kujua ikiwa matoleo yanatolewa kwa muhubiri.

"Umesema unataka noti mpya? Usimseme Mungu vibaya.Yeye si mdogo na hapendi pesa taslimu. Pesa ni yake. Unataka tujiunge na kuwa  vibaraka tuseme Amina. Neno lenye Nguvu kama haliko katika Bibilia si neno."

Haya yanjiri siku chache baada ya Pasta T kuwakosoa wanasiasa ambao wanaenjoi maisha huku rai wakihangaika na hali ngumu ya maisha.

Pasta T,alionyesha kutoridhika wakati amabapo mwanasiasa anatumia takriban sh 420,000 kwa pombe,hisia ambazo zilionekana kumlenga Karen Nyamu.

Pasta T,alivuma kwa mitandao ya jamii,kwa kueleza kutokubaliana na taratibu za ulipaji mahari kwa wanawake.

Katika mahojiano yake ya hivi majuzi,Pasta T,alieleza wazi jinsi alivyochukia  dhana ya kumwekea mwnamke bei,akitoa msimmo wake.

"Nakuja kwa huyu mdada,naambiwa dhamana yake ni  iasi fulni cha hela au mali, kuonyesha kwamba namnunua."Alisema.

Akizungumza kama mume,Pasta T aieleza jinsi wakati wa mazungumzo ya mahari,watu binafsi wakati mwingine uhisi kulazimishwa kutathmini thamani ya mwanamke kwa kulinganisha thamani yake na mifugo na bidhaa nyinginezo.

Akisema hili lineweza kuchangia kupunguza thamana na heshima ya mwanamke katika ndoa.

Akiendele kuzungumza alieleza kuwa mazungumzo ya mahari mara nyingi,hufananishwa na shughuli za kibiashara.

"Baadhi ya hivi vitu tunfanya vinaonyesha ni kana kwamba tunanunua watu,nimewazia swala la kulipa mahari na nahisi kwamba huenda mwanamke akfanyiwa mambo mabaya kwa sababu unahisi kwamba ulimnunua."

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved