Msanii maarufu wa Afro beats kutokea Nigeria, Davido na mkewe Chioma wameripotiwa kubarikiwa na watoto mapacha ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kifo cha mwanao wa kipekee wa kiume, Ifeanyi.
Huku maelezo Zaidi kuhusu taarifa hizo njema yakiwa bado hayajawekwa wazi, madai yanasema kwamba Chioma alibarikiwa na watoto mapacha, mvulana na msichana usiku wa Octoba 9.
Taarifa kutoka nchini Nigeria ziliambatganishwa na ujumbe wa msanii huyo kwenye Twitter akisema kwamba hii huenda itakuwa wiki nzuri sana katika maisha yake na pia ufichuzi uliofnywa kwenye mtandao wa Facebook na mchungaji mmoja kwa jina Evangelist Gospel Agochukwu.
Mchungaji huyo alishiriki kile kilichodhaniwa kuwa ni mazungumzo yake na Davido kupitia mtandao wa WhatsApp.
Katika mazungumzo hayo, Davido alionekana kumdokezea mtumishi wa Mungu kwa furaha kwamba mkewe Chioma alibarikiwa na watoto mapacha akisema, “Tumezaa mapacha. Tumezaa mvulana na msichana. Baddest to the world.”
Ikiwa hiyo haitoshi, Mwimbaji huyo alizidisha uvumi huo baada ya kudokeza kuwa mke wake kuwa ‘Mama Ibeji’ (mama wa mapacha) katika moja ya nyimbo zake kwenye Albamu yake, Timeless.
Katika wimbo unaoitwa ‘In The Garden’, ambao amemshirikisha Morravey, Davido katika mashairi yake alisema, “Abi mo Meji, mama Ibeji”.
Kuzaliwa kwa mapacha wao kungekuwa mwanga kwa wenzi hao waliofiwa na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka 3 mwaka jana, Oktoba.