Pongezi za dhati za Judy Nyawira kwa upendo wa mamake usioyumba

Judy sasa anasema kuwa ombi lake kuu ni kutimiza matamanio ya moyo wa mama yake baada ya kuvumilia safari ndefu ya magumu pamoja.

Muhtasari

•Katika mahojiano ya wazi na shirika la Cleaning the Aiwaves CTA,Judy alieleza hadithi ya maisha yake ya utotoni yenye changamoto,zilizotokna na kufiwa na baba yake mwaka wa 2002.

•"Sikuja hapa kwa ajili yangu,sikuja kuzungungumzia juu yangu, nilikuja hapa kwa ajili ya mama yangu."

Judy Nyawira/Instagram
Judy Nyawira/Instagram

Judy Nyawira,ambaye ni mke wa mcheshi,na muigizaji mashuhuri Abel Mutua,ametoa pongezi za dhati kwa mamake kwa upendo alionyesha wakati ambapo Judy alikuwa akipitia hali ngumu.

Katika mahojiano ya wazi na shirika la Cleaning the Airwaves CTA,Judy alieleza hadithi ya maisha yake ya utotoni yenye changamoto,zilizotokana na kufiwa na baba yake mwaka wa 2002.

Nyawira anaeleza kuwa, mama yake alilazimika kutafuta kazi ya kufagia soko la karibu,ili kukimu mahitaji ya kila siku kwa malipo adimu.

Hili lilipelekea Judy pamoja na ndugu zake kulazimika kubadili shule kutoka za kibinafsi hadi za umma.

Judy sasa anasema kuwa ombi lake kuu ni kutimiza matamanio ya moyo wa mama yake baada ya kuvumilia safari ndefu ya maisha magumu pamoja.

"Sikuja hapa kwa ajili yangu,sikuja kuzungungumzia juu yangu, nilikuja hapa kwa ajili ya mama yangu."Alisema.

Nyawira alieleza kuwa azma yake ya kutoka moyoni ni kushuhudia mama yake akifurahi na kuishi maisha yenye amani,utulivu wa fedha,na furaha katika maisha yake yote.

"Ombi langu moja kwa Mungu ni kuishi muda mrefu vya kutosha kumuona mama yangu akiishi maisha anayostahili.Hilo ndilo jambo pekee ninalohitaji,hayo ndiyo maombi yangu.Kuishi muda mrefu katika dunia hii ili  niweze kutimiza matamanio yote ya moyo wa mama yangu,kwa sababu katika miaka yake ya baadaye,anastahili kuishi maisha yaliyojaa amani,pesa,furaha,na maisha laini.Ni jambo pekee ambalo nikitimiza, basi najua kwa hakika nimefanya sehemu yangu."Judy alieleza.

Huku mahojiano yakiendelea mmoja wa washikadau wa CTA,alijitolea kumtumia mama yake Judy pesa ambazo alisema zingemsaidi kuanzisha maisha.

Hili liliibua hisia,ambazo zilimpelekea Judy kumwaga machozi ya furaha,akionyesha kukubali ombi la hela zilizotumwa kwa mama yake.

Baadaye waliweza kutoa namba ambayo wale ambao wangetaka kumsaidia mama kuanza maisha ya furaha kushiriki mchango wao.