Mmoja wa wasanii maarufu nchini Tanzania Zuchu ambaye pia wasebasi wanadai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond Platinumzs amekiri kutojishughulisha na malezi ya watoto wa Diamond.
Nyota huyo wa nyimbo za Bongo kupitia mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao amesimulia licha ya kuwa ndani ya mahusiano alijua mpenziwe Diamond ana watoto ila kulingana naye jukumu la malezi si lake.
'Kweli nilijua Diamond yuko na watoto na pia wazazi wa kike wa wale watoto wapo kwa hivyo mimi ni kama mwanafamilia tu, mambo ya kuwalea wale watoto ni jukumu la wazazi wao maana wapo na baba yao Diamond kila mara anawaandalia sherehe kwa sababu ni jukumu lake ,alisema Zuchu.
Zuchu alikana madai ya kutengana na mpenzi wake Diamond baada ya siku chache mpenziwe kuonekana na aliyekuwa mpenzi wake Mkenya Tanasha Donnah ambaye walifanikiwa pamoja na mtoto wa kiume.
Zuchu hata hivyo amewataka wasebasi wa mitandao kuwa na subira akitaja swala ya ndoa kutoka kwa mwenyezi Mungu.
"Mitandao ya kijamii inaeneza uvumi mwingi wa uongo kwani wengi wanachochea chuki katika familia ,mimi nimejifuza kutosikiza uvumi kila mara kwani unaweza kufanya mtu akose ladha ya maisha ,nawapenda wale watoto lakini swala ya malezi si langu". alisema