•Kwenye maonyesho ya hivi punde ya tamasha hizo,ubunifu mkubwa wa wasanii umeshuhudiwa jukwaani kutoka kwa wasanii mbali mbali mbao wamedai kuleta mabadiliko kwa sanaa ya muziki na matukio ya kisasa.
Tamasha la Wasafi Festivals 2023, ni mojawapo ya tamasha ambazo zimeandaliwa kwa lengo la kupiga jeki tasnia ya sanaa na talanta za wasanii Afrika.
Tamasha la Wasafi Festival 2023, limetia fora zaidi Afrika na ulimwengu mzima,hivyo kuleta mvuto mkubwa wa wasanii na mashabiki wapenzi wa muziki.
Kwenye maonyesho ya hivi punde ya tamasha hizo,ubunifu mkubwa wa wasanii umeshuhudiwa jukwaani kutoka kwa wasanii mbali mbali mbao wamedai kuleta mabadiliko kwa sanaa ya muziki na matukio ya kisasa.
Wasanii tajika Afrika ambao walipata nafasi ya kuwakilisha nyimbo zao,wameonyesha wazi kuwa kuna matumaini ya kuendeleza tasnia ya sanaa kwenye muziki kwa jini walivyo unda maudhui yao kwenye jukwaa.
Wafuatao ni wasanii na ubunifu walioingia nao kwenye jukwaa kama njia ya kuleta mvuto.
Diamond Platnumz,alifanya vizuri zaidi kwa jinsi alivyoingia kwenye jukua kama mfalme na walinzi wake.Pingine hili linaashiri ni kwa nini anatambulika kama `Simba` wa muziki wa Bongo Flava.
Zuchu naye alionyesha ubunifu wa kipekee.aliingia jukwaani na wenzake wakiwa wamevlia kama wacheza kandanda na hata kucheza kandanda jukwaani. awali kwenye tamasha hilo Zuchu alikuwa ameseti steji kama darasa kisha wakaingia kama wanafunzi. Linavutia, sio!
Lava Lava naye hatamu yake ilipofika,alitokea kwenye steji akiwa amevalia mavazi ya mnyama fulani wa kutisha. Jambo ambalo alipoulizwa wakati akizungumza na Simulizi na Sauti,alisema alitaka kuwa tofauti na wenzake wenye ubunifu wa kuseti steji.
"Kwa kweli Festival inazidi kuwa kubwa sana,na hapa katikati,kulikuwa na kasumba ya kila mtu anawazia seti kwenye steji,kwa hiyo mimi ikabidi niwaze inje ya box,kuonyesha mitindo mbalimbali ya mavazi." Alisema Lava Lava.
Msanii Barnba Mopao naye akaja kwa njia ya kipekee. Mopao kajitokeza jukwaani akiwa amevalia kama mkulima,mikononi kabeba muwa na ndizi. Alidai kuwa watu wa Mtwara ni wakulima hivyoalitaka kuwakumbusha kujishughulisha na shughuli hizo ili kukuza uchumi.
Hatamu za msanii Bill Naz zikawadia naye akatekeleza wajibu wake visawasawa. Bill Naz,kapanga steji kama anayefanya na kampuni ya kusambaza umeme. Maudhui ambayo alisema kayafanya makusudi kwani ana ndoto za kuwa fundi wa kusambaza umeme.
Ubunifu huu unaonyesha jinsi wasanii wanajisatiti kufufua tasnia ya sanaa kwenye muziki jambo amabo limeonekana kupigiwa upato sana na mashabaki kwa jinsi wanavyofurhikia ubunifu huo.