logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Si bibi ya tajiri tena!: Amber Ray adokeza kuachana na Rapudo, ataja dhuluma

"Kwa ajili yangu mwenyewe, lazima nichague mimi."

image
na Radio Jambo

Habari14 October 2023 - 06:49

Muhtasari


• Amber alibainisha kuwa alikuwa akichagua amani na angekuwa sawa hatimaye.

• Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake mitandaoni walihisi ni kiki nyingine ambayo wameamua kuzua.

Keneedy Rapudo ataja ufanisi wa ndoa yake na Amber Ray.

Mwanasosholaiti wa humu nchini Amber Ray amedokeza kuwa mambo si sawa katika penzi lake na mumewe tajiri, Kennedy Rapudo.

Ray baada ya kuacha kumfollow Rapudo kwenye Instagram, alikwenda mbele na kuachia aya ndefu akiashiria kwamba amekuwa akipitia dhuluma za kinyumbani na ameamua kutia kitone katika uhusiano huo kabla dhuluma hazijamfanya kilema.

“Siku zote nimekuwa bingwa wa mapenzi na ndoa, nikijua vyema furaha ya kuwa na familia. Kuwa na watoto wanaokuangalia, kukuthamini na kukuabudu kwa sababu unachoweza kufanya ni kuwapa kile ambacho hujawahi kuwa nacho, pamoja na mengi zaidi. ... Upendo na umoja ambao ndoa inapaswa kusimama juu yake hufifia, na hatimaye, hukuacha ukiwa umechoka." Ray alisema kwenye sehemu ya aya ndefu kwenye Instagram stories zake.

Sosholaiti huyo alidokeza kwamba uhusiano wake na Rapudo ulikuwa wa sumu, na "michubuko na makovu yalizidi ya mwili"

"Kwa ajili yangu mwenyewe, lazima nichague mimi."

Amber alibainisha kuwa alikuwa akichagua amani na angekuwa sawa hatimaye.

"Najua itakuwa siku/wiki nyingi kwangu, lakini afadhali niwe na amani ndani kuliko kujionea uwongo kwa nje. Bora niseme ukweli wangu kuliko kuacha umbea uharibu nilichojenga. mimi na familia yangu kufikia sasa. Mambo katika kaya yangu hayajakuwa sawa... lakini yatakuwa sawa. Familia yangu itakuwa sawa. Na hatimaye, nitakuwa sawa."

Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wake mitandaoni walihisi ni kiki nyingine ambayo wameamua kuzua kwani wawili hao wamekuwa wakijulikana kwa kuzua utani wa kuachana mradi tu waweze kuzungumziwa.

Itakumbukwa kabla ya kuzaliwa kwa mwanao, Rapudo na Amber Ray waliigiza kuachana lakini baadae wakaonekana pamoja pasi na kusema ni kipi kilichowaunganisha tena.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved