Mwanangu alikufa Oktoba 2022 Mungu amenilipa kwa mapacha Oktoba 2023 - Davido ashuhudia

Msanii huyo wa hit ya Unavailable alisema kuwa yeye na mkewe walikuwa wakitetemeka walipogundua walikuwa wanatarajia watoto mapacha.

Muhtasari

• "Ni ngumu sana, watu wengi ambao mambo hayo yamewapata, hautatamani kumwamini Mungu kila katika maisha yako ninayokuambia," alisema.

Davido azungumzia kupata mapacha.
Davido azungumzia kupata mapacha.
Image: Instagram

Msanii Davido anahisi kwamba ni mipango ya Mungu tu ambayo imekuwa ikifanyika katika maisha yake, haswa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kufuatia kifo cha mwanawe wa pekee aliyetajwa kuwa mrithi wa kasri lake, Ifeanyi.

Bosi huyo wa DMW hivi karibuni alikuwa mgeni katika kipindi cha United Masters 005 na mtangazaji Steve Stoute ambapo aliulizwa maswali mengi kuhusu maisha yake, ikiwa ni pamoja na familia yake.

Davido alibainisha kuwa mambo aliyopitia yangeweza kuwafanya watu wengi kuacha kumwamini Mungu lakini bado aliweza kuwa na imani na kuendelea kufanya kile anachopenda kufanya.

Msanii huyo aikiri kujiuliza maswali mengi pamoja na mkewe kufuatia kifo cha ghafla cha mwanao wa kipekee aliyefariki kwa kuzama katika bwawa la kuogelea nyumbani mwishoni mwa Oktoba mwaka jana.

Lakini alikiri kwamba sasa ndio amepata majibu kwamba ni Mungu alikuwa anamtayarisha kwa furaha Zaidi na ya kudumu kwa kumlipa mafungu mawili – watoto mapacha – kama njia moja ya kumlipa kwa kufiwa na Ifeanyi.

"Ni ngumu sana, watu wengi ambao mambo hayo yamewapata, hautatamani kumwamini Mungu kila katika maisha yako ninayokuambia, lakini bado kuwa na imani na kuweza kufanya kile ninachopenda, kuwa na timu kubwa inayonizunguka, inayolenga tu na sasa tunakaribia kumaliza."

Davido pia alizungumza jinsi yeye na Chioma walivyofanya walipogundua kuwa watakuwa na mapacha. Msanii huyo wa hit ya Unavailable alisema kuwa yeye na mkewe walikuwa wakitetemeka walipogundua walikuwa wanatarajia watoto wawili. Alisema yote yalitokea mwezi huo huo wa Oktoba alipompoteza mwanawe Ifeanyi mwaka wa 2022.

“Mimi na mke wangu tulipogundua, tulikuwa tunatetemeka na ilikuwa mwezi huo huo. Mwanangu alifariki mwaka jana Oktoba, mke wangu alijifungua mwaka huu Oktoba hivyo ni mambo.” Alisema.