logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mbona kuweka wazi bila kunijulisha? Vera Sidika alalamika Mauzo kupost mwanao

Brown Mauzo alimtambulisha mwanaye kwa mara ya kwanza kwa mashabiki.

image
na

Habari17 October 2023 - 09:43

Muhtasari


• Vera ambaye alirejea nchini hivi juzi baada ya kukamilisha muda wa likizo yake Marekani,ameshiriki katika ukurasa wake wa Insta,akiuliza sababu za kuchapisha picha za mtoto wao bila ya hata kujulishwa.

• "Ilibidi tu,ila mbona kuchapisha bila hata kunijulisha?"

VERA SIDIKA NA BROWN MAUZO

Mwigizaji na sosholaiti Vera Sidika ameonyesha kutoridhika baada ya aliye kuwa mumewe Brown Mauzo kuchapisha picha za mwanao kwenye kurasa za kijamii zinazoweka uso wake wazi.

Vera ambaye alirejea nchini hivi juzi baada ya kukamilisha muda wa likizo yake Marekani,ameshiriki katika ukurasa wake wa Insta,akiuliza sababu za kuchapisha picha za mtoto wao bila ya hata kujulishwa.

Ila pia alishiriki picha akiwa amembeba mwanaye mkononi ambayo pia iliweka uso wazi na kusema pia hana budi.

"Ilibidi tu,ila mbona kuchapisha bila hata kunijulisha?"

Vera Sidika na mwanao

Alichapisha ujumbe huo huku akiwa amembeba mwanaye mkononi,akimtakia afya njema na baraka za Mungu na kusema atafanya kila juhudi kuhakikisha maisha ya mwanaye yamekuwa  bora.

Brown Mauzo alimtambulisha mwanaye kwa mara ya kwanza kwa mashabiki.

Alishiriki picha ya mtoto wake Ice Brown katika ukurasa wa Insta kwa mara ya kwanza huku akichapisha ujumbe wa kumsifia mwanaye.

"Simba, prince Ice Brown," aliandika 

Chapisho la mauzo linakuja  siku chache baada ya  Vera kutamka maneno ya kumdhalilisha baada ya kurudi nchini kutoka ziara zake marekani

Vera alisema kuwa hawana uhusiano na Mauzo na kumtaka kuwa mbali na yeye akisema hataki kumuona karibu yake.

“Sitaki kumuona Brown Mauzo popote karibu yangu. Nijuavyo, tumeachana, lakini itachukua muda kabla ya talaka kuisha," alisema.

Pia alikanusha madai kwamba Mauzo alionekana na gari lake siku chache baada ya kutangaza kuwa walikuwa wametengana.

"Gari langu lililo na nambari yangu, mtu pekee anayeendesha gari langu ni kaka yangu," Vera alifafanua.

Hata hivyo,hakuna hata mmoja kati ya hawa wawili aliyeshiriki picha zinazoweka wazi uso wa mwanao katika kurasa za mitandao ya jamii

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved