Mtayarishaji wa maudhui Purity Vishenwa almaarufu Pritty Vishy amewataka wanaume wanaomtumia mama yake ujumbe kwenye Instagram.
Huku akimjibu haswa mtumiaji ambaye alionekana kumwandikia mama yake meseji kwenye jukwaa, Vishy aliwaomba vijana wote wanaovutiwa na mama yake wajizuie na kujiheshimu.
"Young boys acheni kumtafuta mama yangu hana pesa za sugar mummy, just have respect jeez. Huyu amekua DM akaona simjibu akamua mamangu ndio konki," aliandika.
Haya yanajiri siku chache baada ya Vishy kuungana na mama yake baada ya miaka 5 .
Katika klipu iliyoshirikiwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, Pritty alinaswa akikimbia kabla ya kumkumbatia mama yake kwa joto. Pritty Vishy alilia huku mama yake akimfariji na kumfuta machozi.
Alifichua kuwa mamake aliondoka nchini akiwa na umri wa miaka 17 na wakati huo alikuwa kidato cha 2.
"Mama yangu aliondoka nikiwa kidato cha 2….ilikuwa ngumu kwani sikuwahi kuwa mbali naye….na mwishowe amefurahi sana🥹😢aaaah Mungu asante sana ☺️ Ninashukuru sana," aliandika.
Katika moja ya ufunuo wake, alifichua kwamba mama yake alikuwa mama kijana.
Alisema wakati mwingine hupata msongo wa mawazo anapofikiria hali halisi ya kujifungua akiwa na umri wa miaka 14 tu na changamoto nyingi zisizohesabika ambazo mama yake alikumbana nazo hadi kumleta katika dunia hii.
“Naona wenzangu wa mama yangu (miaka 35) wana watoto wadogo, wengine wana hata mtoto mmoja na mama yangu ana mimi. Yaani binti mzima mzima ananifanya nijisikie kuzidiwa.