Tunasubiri mwelekeo wa Inspekta Jenerali wa polisi kuhusu suala la Brian Mwenda – Sonko

Mwenda alisisitiza kuwa hana hatia na atajiwasilisha iwapo atatakikana kufanya hivo

Muhtasari

•Mimi si mtoro wa sheria ,Brian aliongeza kwenye video iliyowekwa na Mike Sonko kwenye akaunti yake ya X

Image: Wakili Brian Mwenda anayetajwa kuwa Wakili ghushi katika mahakama

Aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema wanasubiri maelekezo kutoka kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome kuhusu mahali ambapo Brian Mwenda anaweza kurekodi taarifa.

Sonko aliongeza kuwa Mwenda hana makosa yoyote  huku akisema kuwa Mwenda yuko tayari kuandikisha taarifa  na kutokea kortini iwapo watapata thibitisho la kufanya hivyo kutoka kwa    Inspekta Jenerali wa polisi.

Mwenda alisisitiza kuwa hana hatia katika tuhuma hizo na kwamba atajiwasilisha  iwapo atatakikana kufanya hivyo.

   

 

"Kwa rekodi, mimi sio mtoro wa sheria, Brian aliongeza kwenye video iliyowekwa na Mike Sonko kwenye akaunti yake ya X, Mwenda anadaiwa  kuwa wakili ghushi aliyefika mahakamani mara nyingi, akijitambulisha kama wakili wa Mahakama Kuu.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki jana, Mwenda alionekana kortini wakati aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga na wengine walipofika mbele ya mahakama ya Makadara na kumtetea mmoja wa washtakiwa.

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya Eric Theuri pia alitoa wito wa kukamatwa kwa Brian Mwenda.

Theuri, hata hivyo, aliongeza kuwa hawafahamu kesi ambazo Brian aliwasilisha mahakamani kabla ya ufichuzi huo.

"Tunataka kusahihisha taarifa za kupotosha ambazo ziko hadharani kwamba Brian ameshinda kesi 26, kwa kipindi kifupi, haiwezekani kabisa kushiriki katika idadi kubwa ya kesi," aliongeza Theuri.