'Nelly Oaks hajawahi koma kuniita Babe" Akothee asema akiahidi kumpa zawadi

Akothee aliahidi siku moja kumpa Nelly Oaks zawadi ambayo itawashangaza wengi.

Muhtasari

• Aidha, alikiri kwamba Nelly Oaks licha ya kuachana kwa muda mrefu, bado hajawahi koma kumtambua kama ‘Babe’ wake.

Akothee na Nelly Oaks
Akothee na Nelly Oaks
Image: Facebook

Mjasiriamali na msanii Esther Akoth maarufu kama Akothee ameibuka na mapya akisema kwamba aliyekuwa mpenzi na meneja wake Nelly Oaks hajawahi badilisha jina kutoka kumuita ‘Babe’ hata baada ya kuachana takribani miaka miwili sasa.

Akothee alipakia picha ya mwaka 2021 akikumbuka jinsi Oaks alichangia pakubwa katika kumtafutia ubalozi kwenye kampuni moja ambayo alitakiwa kusaini mkataba wa kuweka machapisho 4 tu kwa mwezi na kupata mkwanja mrefu.

Akothee alisema kwamba kipindi Nelly Oaks anamtafutia ubalozi huo, walikuwa wamekosana kidogo kwenye mahusiano yao lakini hilo halikumbadilisha kwani bado alikuwa anamjali.

“Mmm kipindi hiki hata hatukuwa kwenye maongezi 🤔 unajua mahusiano ni kupanda na kushuka @nellyoaks alinipigia simu. Hujambo Babe, nina biashara kwa ajili yako. Je, unaweza kuchukua 1m kwa machapisho manne kwa mwezi ️ Machapisho 4 tu na video 1 ya YouTube. Mimi Yessss,” Akothee aliandika kumbukizi hiyo.

Aidha, alikiri kwamba Nelly Oaks licha ya kuachana kwa muda mrefu, bado hajawahi koma kumtambua kama ‘Babe’ wake, akiahidi kwamba siku moja tu atampa zawadi ambayo itawashangaza wengi.

“Huyu jamaa hajawahi kubadilisha jina langu kutoka Babe na kuwa Esther au AKOTHEE 🤔🤔🤔🤔🤔🤔. Hii ilikuwa 2021. Nitampa @nellyoaks zawadi ambayo itawashtua wengi 🤣🤣🤣🤣🤣” alisema akimalizia kwa kicheko.

Nelly Oaks amekuwa akimpa Akothee shavu la faraja haswa kipindi ambapo msanii huyo alionekana kurukwa na akili kwa kile alikitaja kuwa ni mambo magumu na mazito aliyojionea nchini Uswizi baada ya kwenda kwa kina aliyekuwa mpenzi wake Mr Omosh waliyefunga naye harusi mwezi Aprili mwaka huu.

Katika kipindi cha siku za hivi karibuni, Oaks amekuwa akionekana na Akothee kwenye kila mtoko wa hadhaani, na hivyo kuwafanya mashabiki wake kuhisi huenda wamelitia moto upya penzi lao.

Ndoa ya Akothee na Omosh ilisambaratika mapema mwezi Oktoba licha ya kufunga harusi ya kifahari iliyowavutia wengi mwezi Aprili mwaka huu jijini Nairobi.