logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Professor Jay amvuta Alikiba studioni kwa ajili ya kolabo baada ya kupona

“Unyama ni Mwingi, my two favourite music icons!” mmoja aliandika.

image
na Radio Jambo

Habari18 October 2023 - 07:01

Muhtasari


• “KING anapokutana na KING @officialalikiba 💣💣🔥Studio Session 💪🏻💪🏻Yajayo yanafurahisha sana✍️✍️✍️,” Jay aliandika.

 

Alikiba na Professor Jay

Aliyekuwa mbunge wa Mikumi nchini Tanzania, Joseph Haule maarufu midomoni mwa wengi kama msanii wa rap Professor Jay ametangaza taarifa njema kwa mashabiki wake baada ya ukimya wa takribani miaka miwili ambapo alikuwa amelazwa hospitalini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Professor Jay alipakia picha ya pamoja na msanii maarufu wa Bongo Fleva, Alikiba wakiwa wamesalimiana kwa tabasamu huku wameketi.

Alitangaza kwamba hivi karibuni atafanya ujio mkubwa kwenye tasnia ya hiphop ya Kiswahili na safari hii ngoma yake ya kwanza itakuwa ni kolabo ya nguvu akimshirikisha msanii huyo kutoka Kings Music.

“KING anapokutana na KING @officialalikiba 💣💣🔥Studio Session 💪🏻💪🏻Yajayo yanafurahisha sana️,” Jay aliandika.

Mashabiki wengi walijawa na furaha kumuona Professor Jay amejirudi katika ubora wake na kumkaribisha tena kwenye tasnia ya muziki ambayo alikuwa ameinoa kwa Zaidi ya miaka 20.

“Unyama ni Mwingi, my two favourite music icons!” mmoja aliandika.

“Sasa alikiba umekuwa chukua madini uyo ni level chafu sana Africa na dunia iyo Ndo icon ya bongo fleva uko duniani Ndo akina jay z nasubiri ongeeni nasubiri chupa kali niko pale napata kinywaji baridi sana,” mwingine alisema.

“Siwezi kuogopa kwa hili my big brother @professorjaytz kila nikikukumbuka huwa nakuombea kwamungu uendelee kuwa na afya njema kila itwayo leo so nafurahi sana nikiona maombi yangu mungu anayapokea kwa ukubwa pia naamini sio mimi pekee ninae kuombea ni mamilioni ya watu tuko nawe bega kwa bega natumai kila kitu kinaenda sawa kama tunavyo tamani. All in all tunasubiri kwa hamu ujio wako mpya” Shamnyoka alimpa maua yake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved