logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize aeleza mbona watu walitoroka shoo yake baada ya Sauti Sol kuondoka jukwaani

“Playlist yangu ilianza na nyimbo za shoo za slow mwanzoni, " Harmonize alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 October 2023 - 08:07

Muhtasari


  • • Lakini je, Harmonize kwa upande wake anasemaje kuhusu mashabiki kumtosa na kuondoka pindi tu Sauti Sol walipomaliza?
Harmonize

Wikendi iliyopita, msanii Harmonize alikuwa na shoo yake kwenye ukumbi wa Super Dom Masaki, jiJINI Dar es Salaam ambayo pia ilihudhuriwa na kutumbuizwa na bendi yenye ufanisi mkubwa kutoka Kenya, Sauti Sol.

Katika shoo hiyo, walianza wasanii wengine na baadae Sauti Sol kisha Harmonize akakwea jukwaani kuifunika kabisa, lakini hakuweza.

Katika video ambazo zimekuwa zikienezwa mitandaoni, mashabiki waliokuwa wamejawa na mbwembwe walishangilia Sauti Sol kwa vifijo lakini baada ya zamu ya Harmonize, wengi walionekana kufunga safari na kuanza kuondoka kwenye ukumbi, mmoja baada ya mwingine.

Kuondoka huko kumeibua dhana mbalimbali baadhi wakisema Harmonize alichelewa kuingia jukwaani, ikiwa ni Zaidi ya dakika 20 baada ya Sauti Sol kuondoka jukwaani, hivyo wengi walichoka kumngoja na wakaona bora waondoke tu.

Wengine pia wanahisi kwamba Harmonize alianza na ngoma zenye mwendo wa taratibu wakati Sauti Sol waliacha jukwaa na moto wa nyimbo zao zenye vaibu kama lote.

Lakini je, Harmonize kwa upande wake anasemaje kuhusu mashabiki kumtosa na kuondoka pindi tu Sauti Sol walipomaliza?

Harmonize alianza kwa kujuta kuchukua nafasi ya mwisho kutumbuiza lakini pia anawapiga saluti Sauti Sol kwa kile walichokifanya kwenye jukwaa ambacho yeye mwenyewe kilimshinda kuhimili kupelekea mashabiki kuondoka.

“Kwenye shoo yangu wiki jana, nilipangwa niwe wa mwisho kama ilivyo jadi, tena siku hizi nitaanza kukataa kumaliza shoo maana haya ndio malipo ya kuwa mkarimu. Nimepanda jukwaa 3:45am ukiachilia mbali matatizo ya kiufundi ambayo ni kawaida kutokea, Sauti Sol ni moja ya bendi nzuri kuwahi kutokea Afrika. Walijitahidi sana na nilipenda, kila mtu alifurahi,” Harmonize alianza kwenye aya ndefu.

Harmonize pia alikiri kwamba alianza na nyimbo za mwendo wa polepole lakini pia akakiri kwamba kitendo cha BFF wake Hamisa Mobetto kutotokea kilichangia pakubwa katika kuliuwa vaibu lake.

“Playlist yangu ilianza na nyimbo za shoo za slow mwanzoni, kitendo cha BFF kutotokea kilinikata pia. Wakati mwingine sitawaambia nimemualika yeyote,” Harmonize alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved