Staa wa Bongo, Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz aliwasili na familia yake kamili katika hafla ya Tuzo za Trace 2023 ambayo ilifanyika jijini Kigali, Rwanda Jumamosi jioni.
Video na picha za hafla hiyo iliyopambwa na mastaa kutoka sehemu mbalimbali za bara Africa zinaonyesha bosi huyo wa WCB akiwasili kwenye eneo la tukio huku akiwa ameshikana mikono na watoto wake watatu; Latifah Dangote, Prince Nillan na Naseeb Junior.
Walioandamana nao pia ni mama yake Diamond, Mama Dangote na anayedaiwa kuwa mpenzi wa mwimbaji huyo, Bi Zuhura Othman almaarufu Zuchu.
Sita hao ambao wote walikuwa wamevalia mavazi ya kipekee waliingia ndani ya ukumbi wa tuzo huku wakiwa wameshikana mikono, pengine kuashiria wao ni familia. Zuchu na Tiffah walivaa nguo nyeupe huku Diamond na wanawe wawili wakiwa wamevalia nguo za kijani. Mama Dangote kwa upande wake alivalia kitenge cha njano na nyeupe.
Staa mwenzake wa bongo fleva, Juma Jux naye alitembea nyuma ya familia ya Platnumz pamoja na mpenzi wake wa sasa Karen Bujulu.
Suala la Zuchu kuingia pamoja na familia ya Diamond ilionekana kuwavutia wanamtandao wengi ambao waliona ni ishara tosha kuwa hiyo ndiyo familia yake bora.
Tazama maoni ya baadhi ya mashabiki kuhusu tukio hilo:-
@mymelaninbeautiful: Familia nzima.
@zuchu_lioness: Zuchu looking asome ������������, love the fit, video nzima os wholesome love inashinda ���������������
Official_maggy: Waoooooo my zuuuuuuu❤️❤️❤️❤️❤️❤️
@mtakondasana: Tiffah ni binti wa kifalme nillan mlinzi kaka Nj ndiye mtoto wa dhahabu.
@nattystyles_ : Latifffa anawakilisha familia ya dangote ������
Wakati wa utoaji tuzo, bosi huyo wa WCB alinyakua tuzo ya Msanii Bora Afrika Mashariki na pia akapiga shoo ya kusisimua jukwaani.
Staa huyo wa Bongo alisafiri hadi Kigali siku ya Ijumaa akiwa ameandamana na familia yake. Ijumaa jioni,alipakia video zake, watoto wake watatu na mama yake wakielekea uwanja wa ndege kwa gari lake la kifahari.
Msafara wa magari mengine ya kifahari yaliwasindikiza walipokuwa wakienda kupanda ndege yake binafsi kuwapeleka Rwanda.
“Kigali, Rwanda one time for the @traceawardsfestival,” Diamond aliandika chini ya video yake akiwa na watoto wake ndani ya ndege ambayo alipakia Instagram.