Unaita bwana ya wenyewe 'Muevelasting'-Nyamu ajibizana na shabiki mtandaoni

Katika kujibu kwa haraka, Karen Nyamu na maoni ya kejeli alikanusha kuwa hakuwa akimrejelea Samidoh na kwamba alikosea.

Muhtasari

•Katika chapisho hilo Karen Nyamu alimtaja Samidoh kama "mwenye hasira kali" jambo ambalo lilimkasirisha shabiki aliyejibu madai kuwa yeye ni mnyakuzi wa mume.

•"Nilifurahishwa sana na Arteta, leo tupige pole  pole,tusipigwe kama  Man City na Man U kwa sababu muevelarsting ni timu ya chelsea” 

Seneta Karen Nyamu/Instagram
Seneta Karen Nyamu/Instagram

Seneta wa kuteuliwa, Karen Nyamu alichapisha kwenye  ukurasa wake wa Facebook kuipongeza  Chelsea kwa kutoka sare na Arsenal.

Mwanasiasa huyo  alifarijika kwamba timu hiyo ya Chelsea hawakuicharaza Arsenal kwa vile Samidoh ni shabiki wa Chelsea.

Katika chapisho hilo Karen Nyamu alimtaja Samidoh kama "mwenye hasira kali" jambo ambalo lilimkasirisha shabiki aliyejibu madai kuwa yeye ni mnyakuzi wa mume.

"Nilifurahishwa sana na Arteta, leo tupige pole  pole,tusipigwe kama  Man City na Man U kwa sababu muevelarsting ni timu ya chelsea” Karen Nyamu aliandika.

Shabiki mmoja kwa jina,Murugi Mwinjah,pindi tu alipoona chapisho hilo alimshambulia Nyamu,kakisema atawezaje kumuita bwana ya mtu ivo.

“Ni bwana ya wenyewe unaita mueverlasting??? Team blue” Murungi Mwinjah alichapisha maoni yake kujibu Nyamu.

Katika kujibu kwa haraka, Karen Nyamu na maoni ya kejeli alikanusha kuwa hakuwa akimrejelea Samidoh na kwamba alikosea.

Wakosoaji wengine walidai kuwa mwimbaji huyo wa Mugithi hatimaye angemwacha na kurudi kwa Edday Nderitu na watoto wake.

"Ilikuwa siku ambayo Edday alikutana na Karis mtoto wa daktari kutoka kitui,,,😏😏 kitakuramba😏😏😏😏" shabiki aliandika.

“Usiseme meverlasting......sema Nimsnatching...... nafikiri utaona hii🙈🙈🙈🙊🙊🙊” Shabiki mwingine aliandika.

Mashabiki hao waliendelea na kumtania Nyamu huku wakimrushia maneno cheche za maneno amabyo yanapinga uhusiano wake na Samidoh

"Muevelasting my foot...hizo ni ndoto za mchana...lakini hata kama wewe ni mwakilishi ni Mungu atakuhukumu tu.." Shabiki alimkosoa.

Karen Nyamu kwa muda sasa amekuwa akiibua mijadala mitandaoni tangu kujihusisha kwake na Samidoh.

Hata hivyo,Nyamu alikwenda mbele kutangaza kwamba hatashiriki mume wake na mtu mwingine yeyote na alikuwa akipata nguvu kutoka kwa imani yake ya moyo ili kukabiliana na misukosuko yote.