Wazazi hawafai kuingilia uhusiano wa kimapenzi wa wanao - Wema Sepetu

Talaka nyingi za wachumba uchangiwa na muingiliano wa familia zao

Muhtasari

•Wema Sepetu muigizaji mashuhuri alitoa kauli hii kwa waskilizaji wake katika kituo cha Radio Furaha FM nchini Tanzania wakati ambapo mmoja wa waskilizaji asimulia jinsi ambavyo wazazi wake  walikataa mahusianio  yake na mchumba wake

Wema Sepetu
Image: Instagram

Kulingana na kauli ya Wema Sepetu Wazazi hawana ruhusa ya kutenganisha mahusiano ya wanao  kwani jambo hili hufanya wengi kuishi kujutia jambo hilo,akidokesa kwamba mapenzi ya wachumba wawili wa kuyatenganisha ni wao wenyewe kwa maamuzi yao.

"Wazazi hawafai kamwe kumchagulia mwanao mchumba ambaye wao wenyenye ndio wanataka awe kwa mahusiano, wakati huu wa kidigitali muhimu ni wazazi wawe mfano mwema wakati wanao wanapowaletea wachumba wawabariki tu na kuwafuza jinsi ya kuishi".alisema.

Wema Sepetu muigizaji mashuhuri alitoa kauli hii kwa waskilizaji wake katika kituo cha Radio Furaha FM nchini Tanzania wakati ambapo mmoja wa waskilizaji asimulia jinsi ambavyo wazazi wake  walikataa mahusianio  yake na mchumba wake.

Kwenye mahojiano haya Wema alisema kwamba jambo ambalo hufanya familia nyingi kuingilia swala ya ndoa ya wachumba wawili ni tamaa ya Mahari akisema jambo hili huchangia talaka nyingi kwani wachumba wengi huingia kwa ndoa kwa maaumuzi ya wazazi ila si kwa maamuzi yao wenyewe.

"Kwa wazazi komeni kabisa wapeeni wanao fursa ya kufuraiha ladha ya ndoa msiingilie kamwe, ndoa ni baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu cha muhimu muoneshe upendo kwa wanao wanapo chumbiani  ili wawaletee baraka za wajukuu".alisema muigizaji Wema.