Siku chache baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwa mtagazaji na mshauri wa vijana na wanandoa kwenye kituo cha Radio Wema Sepetu amesema kuwa amechukulia jukumu hilo kwa uzito.
Nimeamua kuchukulia jukumu langu la kutangaza kwa Radio kwa uzito ni kauli aliyochapisha kwenye mtandao wake wa instagram kwenye picha yake aliyokuwa ameshikilia kijiradio.
Muigizaji huyo wa muda mrefu nchini Tanzania alikabidhiwa nafasi ya kuhudumu kama mtangazaji wa vipindi vya mapenzi vinavyohusisha vijana kwa kuwapa ushauri ufaao kwa kuwashauri.
Muigizaji huyu amekuwa akifanya vipindi vya ushauri kwa kushirikisha waskilizaji ambao wanasimulia changamoto wazakumbana nazo huku Sepetu akiwapa ushauri.
Siku chache zilizopita kwenye mahojiano ya moja nyota huyu wa cinema za Bongo alifunguka na kusema kwamba alichagua kituo hicho kuelimisha watu wengi ambao wanapitia wakati mgumu kwenye familia zao na pia kwenye ndoa zao.
Mkuu wa kituo hicho baada ya kuhojiwa alifunguka na kusema kuwa walimchagua wema kwa kuwa alikuwa mfano mzuri kuigwa na waskilizaji kwani ni nyota mashuhuri anayetabuliwa na vizazi vingi.