Msanii wa kike kutoka Tanzania, Saraphina maarufu kama Phina amemjia juu mpenzi wa Rayvanny, Fahyvanny kwa kauli yake kuwapikia upato warembo wenye rangi nyeupe za ngozi kupata mapenzi ya wanaume mara dufu ikilinganishwa na wenzao weusi.
Phina alitoa tamko la kumjibu saa chache tu baada ya Fahyvanny kudai kwamba ukweli ni kwamab wanaume wengi hata ndani ya nafsi zao wakiulizwa kuchora taswira ya wanawake wanaowawazia kuwaoa au kutoka nao kimapenzi basi sharti wataje weupe wa ngozi.
Kwa mujibu wa Phina, rangi ya ngozi nyeupe haina thamani yoyote kwani siku hizi warembo wengi huinunua katika maduka ya vipodozi lakini ngozi nyeusi huwezi kuipata popote kwa hiyo nit ya bei ghali kuliko vile ambavyo wengi wanafikiria.
“Ngozi nyeusi wewe ni expensive asikuambie mtu. Kwa sababu huwezi kuipata dukani unaitolea wapi? Rangi nyeupe watu wananunua, lakini nyeusi ushawahi kuona wapi wewe ikiuzwa? Kwa hiyo maanake ni kitu ambacho kiko priceless,” Phina alisema.
Mrembo huyo alikwenda mbele akisema kwamba kauli ya Fahyma ni ya kipuuzi akisema kwamba huenda alikuwa anajizungumzia mwenyewe kutokana na biashara lakini si uhalisia.
“Kwa wanawake ambao wana ngozi nyeusi nyinyi jivunie kwa sababu ni kitu ambacho huwezi kukipata popote. Mimi nafikiri san asana yeye alisema kwa sababu ya biashara,” Phina alisema.
Awali tuliripoti kwamba mrembo Fahyvanny alisema tena kwa msisitizo kwamba wanawake weupe wana nafasi kubwa sana ya kupata mapenzi ya wanaume kwa haraka bila kuhangaika ikilinganishwa na wenzao weusi.
“Unapendwa lakini sasa tukubali au tukatae ni kwamba wasichana weupe wanapendwa Zaidi. Sina maana mbaya lakini hata mwanamume yeyote yule aliye na mwanamke mweusi ndani yake aliyekuwepo ni mweupe,” Fahyvanny alisema.
Msanii Phina alijizolea umaarufu kama miaka miwili iliyopita baada ya kibao chake cha ‘Nipo nyonyo nipo titi’ kuteka anga nchini Kenya na Tanzania na kuwavutia mashabiki wengi ambao walimtaja kama malkia wa kuweza kujaza pengo la msanii wa muda mrefu Lady Jaydee kama malkia wa Bongo Fleva.