Watu wengi hudhani mimi ni wazimu - Embarambamba

Madaktari walinifanyia utafiti ili kudhibitisha akili yangu ni timamu, Embarambamba aeleza.

Muhtasari

•Embarambamba alizua minong’ono mitandaoni wiki chache zilizopita kwa kibao chake cha ‘Nataka Kunyonywa’ .

• Msanii  huyu kisha alirejea siku chache  na kibao kingine chenye utata kwa jina ‘Panua’.

Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Msanii wa injili mwenye utata kutokana na maudhui ya nyimbo zake, Embarambamba amefunguka na kusimulia jinsi ambavyo watu wengi hudhani yeye ni ana kichaa kwa jinsi ambavyo husakata densi kwenye video za muziki wake.

"Mfumo wa kucheza kwenye matope wakati wa mvua ni jambo la kawaida kwangu watu wengi hudhani nimerogwa huku wengine wakiniambia nimepoteza akili zangu ila kwangu jambo hili nalifanya ili kumtukuza Mungu kwa kumchezea densi", alisema .

Embarambamba alizua minong’ono mitandaoni wiki chache zilizopita kwa kibao chake cha ‘Nataka Kunyonywa’ msanii  huyu kisha alirejea siku chache  baadaye na kibao kingine chenye utata kwa jina ‘Panua’.

Msanii huyu amefichua kwamba kwa wakati mmoja madaktari wa kuchunguza afya ya akili walizuru nyumbani kwake kumfanyia ukakuguzi na kudhibitisha kwamba akili yake ni timamu.

Baada ya mahojiano  msanii huyu alidokeza kuwa Licha ya wengi kuhisi kwamba anaimba mambo ya kutukuza anasa akijificha ndani ya jina la utakatifu, alisema kwamba yeye anaimba injili ila wafuasi wengi ndio wanaomchukulia vibaya wakiwa na fikira za anasa.

Msanii huyu  alisimulia kuwa sehemu ya wimbo huo aliimba akimtaka Mungu kupanua  baraka kwa njia ambayo iliwaacha wengi wakidhani huenda anaimba mambo tofauti na injili.